Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, February 16, 2010

Hela za Fidia Kiwapa zataka kumtokea puani!!!!!!

KIJANA mmoja aliyetambulika kwa la Mbegu Moto amejikuta matatani baada ya kubambwa akijaribu kutaka kuchukua fidia kwa kutumia jina la marehemu baba yake bila kufungua kesi ya mirathi. Sakata hilo liliibuka jana baada ya mtoto huyo kwenda kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa unaotumika kuwalipa fidia wakazi hao akiwa na kitambulisho chenye jina marehemu baba yake, lakini akiwa amebandika picha yake. Akizungumzia hilo mmoja wa wajumbe wa kamati ya malipo alisema nyumba yenye namba KP 996 ilikuwa ikimilikiwa na marehemu Mbegu Moto Bothi ambaye alishafariki na kwamba taarifa za kifo chake zinajulikana kwenye kamati hiyo. Alisema mara baada ya kuwasili kwake Jumatano ya wiki iliyopita kamati hiyo ilimtilia mashaka na kumtaka arudi nyumbani kwake akachukue vielezo vingine na ndipo alipopotokea jana akiwa na katibu wa iliyokuwa serikali ya mtaa ili amtambulishe kwetu. Kutokana na utambulisho aliokuwa nao kamati iliamua kumweka chini ya ulinzi ili kuwezesha hatua nyingine za kisheria kuchukua mkondo wake. "Wakati wa uthamini wa nyumba za Kipawa mzee huyo alikuwa hai ndiyo sababu ya jina huyo marehemu kuingia kwenye kitabu cha malipo na kutengenezewa hundi, baada ya kufariki kwake, serikali ilipata taarifa kamati inalijua hilo na ndio maana ilisita kumpatia hundi kijana huyo,"alisema mmoja wa wajumbe wa kamati. Alisema jambo hilo liliishitua kamati hali iliyowalazimu kuhoji sababu za kijana huyo kwenda kuchukua hundi hiyo ambayo baadaye ilifahamika kuwa ni ya baba yake mzazi aliyefariki muda mrefu uliopita. Akizungumzia hilo katibu wa iliyokuwa serikali ya mtaa wa Kipawa Said Hangahanga alisema yeye anaifahamu familia hiyo, lakini hakujua kama kijana huyo alikwenda kuchukua fidia hizi bila ya kufungua kesi ya mirathi. Alisema yeye alipoitwa na kamati alijua kuwa anakwenda kufanya kazi ya kuelezea namna anavyomfahamu kijana huyo kama watu wengine wanavyofanyiwa pindi kunapokuwa na ugumu wa kamati kuwatambua. "Mimi ninaifahamu familia ya mzee Mbegu ina watoto watatu na huyu ndiye mkubwa, kimsingi sielewi ni kwani hakufungua kezi ya mirathi labda aliona apite njia ya mkato ili apate fida hizo,"alisema Hangahanga na kuongezea "yeye ndiye anayetegemewa na familia yake ukisema anaiba anamuibia nani au anajiibia?"alihoji. Alisema yeye alikwenda kutoa taarifa ya namna anavyomfahamu, lakini ahakuwa anajua kama kijana huyo kapitia njia ya mkato kiasi hicho katika madai yake.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote