Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Wednesday, February 10, 2010

Mungu si Athumani - Aokolewa baada ya kuishi chini ya ardhi kwa siku 27 bila ya kula wala kunywa!!!

Miujiza imetokea nchini Haiti kwa mwanaume ambaye alikuwa hana chakula wala maji kuweza kuokolewa toka kwenye kifusi cha jumba alilokuwemo siku 27 baada ya kufunikwa na kifusi cha jengo hilo wakati tetemeko kubwa la ardhi lilipotokea nchini Haiti. Madaktari nchini Haiti wanampatia matibabu mwanaume mwenye umri wa miaka 28 wa nchini Haiti ambaye ameokolewa toka kwenye kifusi cha jengo alilokuwemo siku 27 baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuikumba Haiti januari 12 mwaka huu.Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Evans Monsigrace, aliokolewa jana jumanne na aliwaambia madaktari kuwa alifunikwa na kifusi cha nyumba aliyokuwemo wakati alipokuwa akipika wali."Kimaajabu ameweza kuishi 27 chini ya kifusi cha nyumba yake", alisema daktari Dushyantha Jayaweera, mganga mkuu wa hospitali aliyolazwa mwanaume huyo.Kwa mujibu wa mama yake Evans, Evans aliokolewa baada ya kugunduliwa na watu waliokuwa wakiondoa kifusi cha nyumba hiyo.Dokta Jayaweera alisema kuwa Evans alioneka kuwa dhoofu sana na kama amechanganyikiwa vile lakini ogani zake zote zilionekana kuwa salama.Evans aliwaambia madaktari kuwa aliishi chini ya kifusi kwa muda wote huo bila maji wala chakula na kuwafanya madaktari watume wataalamu kwenye eneo alilookolewa kuthibitisha madai yake.Wataalamu hao walishindwa kugundua uwepo wa maji au chakula kwenye eneo hilo na kuwafanya madaktari waumize vichwa wasijue imekuwaje Evans ameweza kuishi siku zote hizo bila kula wala kunywa maji."Tukio lake limetufanya tuanze kufikiria upya yale tuliyokuwa tukiyajua kuhusiana na mwili wa binadamu", alisema dokta Jayaweera.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote