Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Friday, February 12, 2010

Nguza, Papii Kocha ndo basi tena uraiani???????? Francis ana Mbangu huru

VILIO na majonzi jana vilitawala katika Mahakama ya Rufaa Tanzania jijini Dar es Salaam wakati mahakama hiyo ilipomuamuru mwanamuziki maarufu, Nguza Viking maarufu kwa jina la Babu Seya, na mwanawe, Papii Nguza (Papii Kocha) waendelee na vifungo vya maisha jela. Kwa mujibu wa taratibu za mahakama Tanzania, uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ni wa mwisho, hivyo Babu Seya na Papii Kocha watakaa jela maisha yao yote. Mahakama hiyo imewaachia huru watoto wa Babu Seya, Nguza Mbangu na Francis Nguza. Tangu Juni mwaka 2004 Babu Seya na wanawe watatu walikuwa jela kutumikia kifungo cha maisha kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam iliona wana hatia ya kubaka ya kulawiti. Kwa mujibu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Babu Seya na Papii wamekutwa na hatia katika baadhi ya makosa, lakini Francis na Nguza Mbangu hawana hatia katika kosa lolote. Baada ya Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Neema Chusi, kusoma hukumu hiyo ya rufaa, watu walianza kulia, sauti ya Francis ilisikika zaidi pengine kutokana na uchungu wa kumuacha baba na kaka jela,sanjari na furaha ya kuachiwa huru. Wakati Francis akiendelea kulia, watu wakiwemo waaandishi wa habari walimzunguka hivyo kusababisha wananchi wengine waliokuwa pembeni kulia, askari wakawa wanabubujikwa machozi. Baada ya hukumu hiyo,wanamuziki hao walitolewa katika chumba cha mahakama na kupelekwa katika chumba kingine kilichozungukwa na watu wengi wakiwemo wasanii waliokwenda kusikiliza hukumu hiyo. Wakati wakielekea katika chumba hicho Papii Kocha alisikika akisema “Kikwete atatusaidia, Kikwete atatusaidia”. Chusi amesema, mahakama imeshindwa kuwatia hatiani Francis na Nguza Mbangu kwa sababu upande wa mashitaka umeshindwa kudhibitisha makosa dhidi yao. Mahakama imetoa mfano kuwa, baadhi ya mashahidi waliopelekwa mahakamani na upande wa mashitaka waliweza kuwatambua Papii Kocha na Babu Seya lakini hawakuwatambua hao wengine hata kwa majina. Awali Babu Seya na wanawe watatu walihukimiwa katika mashitaka 23, Mahakama ya Rufaa imeyaondoa mashitaka 11 ya kuingiliwa kinyume kwa maumbile kwa sababu hakuna mashitaka kama hayo chini ya sheria za kujamiiana. Mahakama ilikubaliana na Wakili Mabere Marando kuwa ushahidi uliotolewa ulichukuliwa bila kiapo kwa vile hakimu hakujiridhisha kama watoto waliohusika walikuwa na uelewa wa kutambua kile walichokuwa wanakisema ni cha kweli na hivyo ushahidi huo ulitakiwa kuungwa mkono. Mahakama hiyo imebaini kwamba,kulikuwa na ushahidi wa kutosha wa kuunga mkono ule wa watoto, ukiwemo unaoelezea namna chumba kilivyo ambacho kilikuwa kinatumika kwenye ubakaji na pia kitendo cha Babu Seya kuongeza sauti ya redio wakati wa kutenda kosa ili watu waliokuwa nje wasifahamu kilichokuwa kikiendelea ndani. Juni 25, 2004, Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu, Hakimu Addy Lyamuya, aliwatia hatiani Babu Seya na wanawe watatu kwa makosa 23 ya ubakaji na ulawiti, akawahukumu kifungo cha maisha. Wasanii hao walibainika kutenda makosa 10 ya kubaka watoto wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huo huo kati ya April na Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza kwa Remmy, Dar es Salaam. Waliwasilisha rufaa kwenye jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania akiwemo Mbarouk Salim, Salum Massati na Nathalia Kimaro. Katika rufaa hiyo, wakili wa wasanii hao,Mabere Marando, alidai kuwa,Hakimu Lyamuya, aliingiza maslahi yake binafsi na hakuwa akizingatia ushahidi uliokuwa ukitolewa na upande wa washitakiwa. Marando amedai kuwa, hakimu huyo alitoa kipaumbele kwa mashahidi wa upande wa Jamuhuri na kupuuza mashahidi wa upande wa washitakiwa hivyo kuwanyima haki. Kwa mujibu wa Marando, watoto wote waliokwenda mahakamani kuthibitisha kwamba walibakwa au kulawitiwa na washitakiwa walitoa ushahidi bila kiapo isipokuwa mmoja kati ya 10 waliotoa ushahidi. Amedai kwamba, watoto hao pia hawakurekodiwa ushahidi wao kabla ya kutoa ushahidi mahakamani jambo ambalo linakiuka sheria. Marando amedai kuwa,baadhi ya watoto waliotoa ushahidi walikiri kutomtambua Babu Seya na washitakiwa wengine na kwamba, ripoti ya Daktari ilionyesha kwamba miongoni mwa watoto hao walikuwa ni bikira hivyo kumaanisha kwamba walikuwa hawakufanya kitendo chochote kilichohusiana na mashitaka hayo.

1 comment:

Unknown said...

Hamna haki Tz....So unfair to Babu na Papii. Hii kesi nzima inanuka ufisadi.

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote