Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, February 2, 2010

Habari njema kwa Waislamu duniani

Mshine hiyo imevumbuliwa na kampuni ya nchini Malaysia ya AACE Technologies kwaajili ya kuwasaidia waislamu kutia udhu bila kutumia maji mengi.Mashine hiyo inatumia misingi yote ya sheria za kiislamu katika kutawadha na imepitishwa na serikali ya Malaysia kutumia kuwatawadhisha watu.Mashine hiyo yenye urefu wa mita 1.65 inayojulikana kama "The Auto Wudu Washer" inatumia mabomba yenye sensor kumtawadhisha mtu mmoja katika hali ya kusimama kwa kutumia lita 1.3 tu.Mashine hiyo itasaidia kupunguza upotevu wa maji wakati wa kutawadha ambapo kawaida bomba huachwa wazi muda wote wakati wa kutia udhu, alisema mwenyekiti wa AACE, Anthony Gomez.Kuna waislamu zaidi ya bilioni 1.7 duniani ambapo asilimia kubwa ya waislamu wapo Afrika na mashariki ya kati ambako kuna uhaba wa maji.Mashine hiyo imepokelewa vizuri katika nchi tajiri za kiarabu ambazo zimeelezea mpango wa kuzinunua mashine hizo.Mashine hizo mbali ya kumtawadhisha mtu, humwezesha mtu anayetawadha kusikiliza quran huku akitawadhishwa."Wakati wa Hija, watu milioni 2 hutumia lita milioni 50 za maji kwa siku moja kwaajili ya udhu, kwa kutumia mashine hizi wangeweza kuokoa lita milioni 40 kwa siku", alisema Gomez.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote