Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, February 2, 2010

Daktari wa Marie Stop mbaroni kwa kudaiwa kubaka mgonjwa

DAKTARI wa Hospitali ya Marie Stoppers iliyopo Mwenge, jijini Dar es Salaam, Paul Andrew ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kudaiwa kumbaka mgonjwa aliyefika hospitalini hapo wakati akimpatia matibabuIlidaiwa kuwa mgonjwa huyo alifika hospitalini juzi, majira ya jioni kwa lengo la kupatiwa matibabu wakati alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tumbo na alifika kwa ajili apatiwe uchunguzi wa kina ili tatizo lake liweze kugundulika.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga alithibitisha kuwa mgonjwa huyo alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kina wa tumbo llilokuwa likimsumbua.Alisema alipofika hapo alikutana na daktari huyo aliyetambulika kama Dk. Andrew na alimwandikia afanyiwe kipimo cha Utra Sound ili aweze kugundulika tatizo lake. Kalinga alisema alithibitisha tukio hilo kwa mujibu wa maelezo ya mgonjwaAlisema baada ya mgonjwa huyo kuingia katika chumba cha kufanyiwa kipimo hicho ndipo daktari huyo alimpa kitu kilichomfanya alale kwa muda na nguvu ya dawa ilipokwisha alishtuka na kumkuta daktari huyo akiendelea kumbaka. Alisema mgonjwa huyo alipozinduka na kujikuta akibakwa na daktari huyo alijinasua na alitoka nje na kukimbilia Kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama na kufungua jalada lenye namba RB/KJN/123/552/10. Alisema mgonjwa huyo aliongozana na askari wa kituo hicho hadi hospitalini na kumkamata mtuhumiwa aliyekuwa bado yupo eneo hilo. Kamanda Kalinga alizidi kutoa maelezo hayo kuwa, kutokana na maelezo ya utatanishi wa mgonjwa huyo ilibidi jeshi hilo apelekwe kufanyiwa vipimo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kubaini kama kweli alifanyiwa unyama huo. Baada ya vipimo kufanyika iligundulika alifanywa na mtuhumiwa anashikiliwa na polisi

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote