

Siku chache baada ya kutoa habari zilizoanika rushwa zinazofanywa na askari wa kikosi cha usalama barabarani, mwandishi wa habari za uchunguzi, Jerry Muro (
mwenye tshirt ya njano pichani) ameingia matatani baada ya kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa, Murro ambaye ni mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji (TBC) na ambaye amejipatia umaarufu kutokana na kufichua aina tofauti za rushwa, anashikiliwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi ambayo imeeleza kuwa habari zaidi kuhusu mkasa wake zitatolewa rasmi. Muro alikumbwa na mkasa huo majira ya saa 6:00 jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Sea Cliff. Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata, Muro alikamatwa baada ya kuwekewa mtego na polisi mara baada ya kuarifiwa na mfanyabiashara mmoja, ambaye jina halijawekwa bayana na polisi, kuwa mwandishi huyo amedai rushwa ya Sh10 milioni inasemekana mwandishi huyo alikamatwa muda mfupi baada ya kukabidhiwa fedha hizo. "Muro alikuwa ameahidiana na mfanyabiashara mmoja kuwa angepewa Sh10 milioni kama hongo, Kamanda wa polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alikiri jeshi lake kumshikilia mwandishi huyo kwa mahojiano, lakini hakutaka kuelezea zaidi mkasa huo. "Ni kweli yuko hapa na anahojiwa na mimi ndo ninapewa taarifa hivyo nitatoa taarifa kamili kesho (leo) saa 6:00,"alisema Kova.
No comments:
Post a Comment