Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, February 1, 2010

Nani alaumiwe? Zuma au?

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amepata mtoto wa 20 baada ya kumpa mimba binti wa rafiki yake wa karibu ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kombe la dunia nchini Afrika Kusini.Gazeti la Sunday Times la Afrika Kusini limeripoti kuwa Zuma alimpachika ujauzito Sonono Khoza ambaye ni binti wa Irvin Khoza, mmiliki wa timu ya Orlando Pirates.Sonono mwenye umri wa miaka 39 alijifungua mtoto wa rais Zuma mwezi oktoba mwaka jana.Kwa mujibu wa gazeti hilo, baba yake Sonono amehuzunishwa sana na kitendo cha Zuma kumtia mimba binti yake.Khoza aliiambia familia yake kuwa anahisi amesalitiwa na Zuma ambaye alikuwa akimchukulia kama rafiki yake wa karibu sana.Gazeti hilo liliendelea kusema kuwa mwezi disemba mwaka jana, wawakilishi wa rais Zuma waliitembelea familia ya Khoza katika mji wa Soweto na kujadiliana nao malipo ya kitamaduni ya kumzalisha mwanamke nje ya ndoa (inhlawulo).Rais Zuma alikutana na Sonono na mama yake mwanzoni mwa mwezi huu kulijadili zaidi suala hilo.Zuma hivi sasa anaishi na jumla ya wake watatu na amewahi kufunga ndoa jumla ya mara ya tano.Mtoto wa Sonono amekuwa mtoto wa 20 katika idadi kubwa ya watoto wa rais Zuma.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote