Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, February 2, 2010

Wamarekani wazuiliwa Haiti

Serikali ya Haiti imewatia kizuizini Wamarekani kumi ambao inasema walikuwa wakijaribu kuwasafirisha nje ya nchi watoto wadogo bila idhini ya serikali. Msemaji wa serikali ya Haiti, Yves Christallin, alisema Wamarekani hao walikamatwa na zaidi ya watoto thelathini kwenye mpaka na Jamhuri ya Dominica, ambako walisema walikuwa na kituo cha watoto yatima. Msemaji huyo alisema Wamarekani hao hawakuwa na hati zinazothibitisha ikiwa watoto hao walikuwa ni yatima kutokana na tetemeko la ardhi lililoikumba Haiti hivi karibuni. Wamarekani hao ni kutoka kanisa lenye makao yake katika jimbo la Idaho. Mchungaji katika kanisa hilo, Clint Henry ameiambia BBC kuwa kundi hilo la Wamarekani limekuwa na hati zote zinazohitajika kufanya shughuli zao.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote