Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Friday, December 18, 2009

Achana Talaka mbele ya mashahidi

MWANAMKE mmoja [jina kapuni] jana alitoa kioja cha mwaka baada ya kupewa talaka na mumewe iliyomtaka arudi nyumbani kwao na yeye kuichana talaka hiyo mbele ya mashahidi na kuiingia ndani kwenda kulala kwa kujiamini. Mtafaruku huo ulitokea jana majira ya jioni, huko maeneo ya Magomeni Makanya baada ya mume wa mwanamke aliyetambulika kwa jina moja la Hamidu kumuandikia talaka moja mke wake huyo kwa madai kuwa alichoshwa na tabia za mke wake huyo ambaye alimuonya bila ya kujirekebisha.Hivyo Hamidu kwa kuwa alichoshwa na tabia za mke wake huyo ambaye alimkanya kwa mara kadhaa bila kumjali hivyo aliamua kuandaa mashahidi ili aweze kumkabidhi talaka hiyo kwa ushahidi.Hivyo aliandaa mashahidi wawili watatu na kuwaeleza na kumkabidhi talaka hiyo ghafla bila kuamini mwanamke huyo alipokea karatasi hiyo na alipoisoma kuwa ni talaka papohapo aliichana mbele ya watu hao na aliingia ndani kwake kwenda kulala na mashahidi hao wakibaki midomo wazi wakikosa la kusema.Akiongea na mwandishi wa habari hii mume wa mwanamke huyo alisema kuwa aliamua kumpa talaka moja mke wake huyo kwa kuwa alikuwa na tabia ya kupenda starehe na alipokuwa akitoka kwenda sehemu za starehe alikuwa anachelewa kurudi nyumbani na kurudi alfajiri kitendo ambacho alikuwa hafurahishwi nacho.Alisema yeye alikuwa anamruhusu mke wake huyo siku moja moja aende kuangalia bendi “live” lakini alikuwa anakerwa na urudiji wake wa kuchelewa na mara nyingine alikuwa akimfata sehemu husika huwa anakuwa mbishi kurudi na kutaka hadi bendi hiyo itakapotangaza kuwa wimbo huu ni wa mwisho na yeye ndiyo huanza safari ya kurudi nyumbani.“Sasa dada yangu mke wa mtu utarudiji alfajiri nyumbani kwake? Embu nisaidie, Alisema mara nyingine anaamua kumruhusu atoke peke yake kwa kuwa huwa amechoka na kumruhusu mke wake huyo atoke mwenyewe siku nyingine huwa wanatoka wote na kusema kwa kuwa mke wake huyo hupendelea sana taarabu lakini yeye hapendi sana basi ndio mana hulazimika siku nyingine amruhusu aende mwenyewe.Akiongea na chanzo chetu kwa njia ya simu mwanamke aliyepewa talaka na kuichana alipotakiwa kujibu tuhuma hizo alisema “ ni kweli nimeichana talaka mana sikuona kosa langu mimi ni nini” “halafu niende wapi na umri huu aanze yeye kuondoka kwenye nyumba ambayo tumejenga wote tukitumia mishahara yetu kwa pamoja mi sikuona kosa languAlipoulizwa kama ni kweli anachelewaga kurudi alisema ni “nadra sana, si siku zote kwanza kwa miezi miwili labda natoka maramoja tu, ujue sikia mimi mume wangu ana wivu sana sasa tunapelekana tu hivyohivyo“ yeye anachotaka mimi nikaege ndani tu bila kujiburudisha sasa akigoma akinikataza siku nyingine na mimi nikiwa na hamu ya kutoka ndipo natoka kibabe, mana yeye huwa anataka atokege yeye bila mimi sasa na mimi kitendo hicho siwezi“Mbona yeye anatoka anaenda FM Academia, Twanga nami namuacha anarudi amechelewa sanaa, na ukimwambia tutoke wote hataki namimi ndio mana naamuaga yeye akienda TWANGA mimi naenda JAHAZI

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote