Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, December 3, 2009

Sophia Simba na Anna Kilango kutunishiana misuli?

UGOMVI kati ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango (CCM), umeingia katika hatua mpya. Wakati Mama Kilango akijiandaa kufungua kesi dhidi ya Waziri Simba akidai kuchafuliwa jina, suala hilo limetinga ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na katika Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam. Kesi hiyo imetinga Ikulu baada ya Mama Kilango ambaye ni mmoja kati ya wabunge apambanaji wa ufisadi, kuandikia barua ofisi ya Waziri Mkuu na katika ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM taifa, kuwajulisha kuwapo kwa kesi hiyo ambayo imeanza kugusa hisia za wengi. Katika barua hizo, Mama Kilango anasema kesi hiyo haitakihusisha chama wala serikali licha ya ukweli kwamba mlalamikiwa katika kesi hiyo (Sophia Simba), si tu kwamba ni waziri, bali pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM. Vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa, wakati Mama Kilango kupitia mawakili wake akimpa Waziri Simba notisi ya siku 14 ya kusudio la kumfungulia mashitaka, waziri huyo kupitia mawakili wake ameijibu notisi hiyo na kumtaka wakutane mahakamani. Waziri Simba katika majibu yake, anadai hajawahi kuitisha mkutano na waandishi wa habari hadi akaririwe na vyombo vya habari vilivyochapisha kauli yake kutoka kwenye kikao cha ndani cha wabunge wa CCM. “Mteja wetu hajapata kuitisha mkutano na waandishi wa habari, wala yeye si mhariri wa habari wala mchapishaji aliyehariri na kuchapisha habari hizo, hivyo hausiki na taarifa za vyombo vyote vya habari vilivyomkariri akimshambulia Mama Kilango,” ilisomeka sehemu ya majibu ya Waziri Simba kwa Mama Kilango. Kutokana na hali hiyo, Waziri Simba ambaye katika siku za hivi karibuni jina lake limekuwa likipasua anga za siasa nchini, alisema kamwe hataomba radhi na kumtaka Mama Kilango wakutane mahakamani. pamoja na mambo mengine katika kesi hiyo, Mama Kilango anadai fidia ya zaidi ya sh bilioni moja kwa kuchafuliwa jina. Inadaiwa kuwa Waziri Simba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM (UWT), alimkashifu Mama Kilango wakati akichangia hoja kwenye kamati inayoongozwa na Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, inayofanya kazi ya kutafuta chanzo na suluhu ya mgogoro wa wabunge wa CCM wenyewe kwa wenyewe na dhidi ya serikali yao. Ingawa Mama Kilango ametaka kesi hiyo isihusishwe na siasa, habari kutoka duru za wanasheria zinasema kuwa kama kesi hiyo itafunguliwa, wajumbe wa Kamati ya Mwinyi, lazima waitwe mahakamani kutoa ushahidi wao. Wajumbe wa kamati hiyo ambao wanaweza kutinga kortini kama mashahidi ni Mzee Mwinyi, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM, Abdulrahman Kinana. Katika hatua nyingine, CCM imeanza vikao na wahusika wa kesi hiyo ili imalizwe ndani ya vikao vya chama kwa madai kuwa inaweza kukichafua zaidi chama hicho. Hivi karibuni kwenye kikao cha Kamati ya Mzee Mwinyi mbele ya wabunge wa chama hicho tawala, Waziri Simba alidaiwa umshambulia Mama Kilango kuwa si msafi kiasi cha kuwatuhumu wenzake kwamba wanahusika na ufisadi. Waziri Simba alikwenda mbali zaidi akisema kwamba baadhi ya watu ambao Mama Kilango anawaita mafisadi leo, ndio waliofadhili harusi yake na Mzee John Malecela. Waziri Simba alikaririwa akisema harusi ya Kilango na Mzee Malecela, ilifadhiliwa na mtuhumiwa wa ufisadi, Jeetu PatelPatel kwa sasa ana kesi katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam akituhumiwa kuiibia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa kuchota takribani sh bilioni 11 kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA). Akijieleza kwenye kamati hiyo, Waziri Simba alimtuhumu pia Malecela ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya pili, kwamba wakati anawania kuteuliwa kugombea urais mwaka 2005, Jeetu Patel alimpa sh milioni 200 kwa ajili ya kampeni. Malecela ambaye wakati huo alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, aliondolewa mapema kwa nguvu ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa hata bila ya kujadiliwa na kikao. Akizungumza kwa kujiamini na ujasiri, Simba alimtuhumu mama Kilango kuwa kelele zote anazozitoa kuwashambulia baadhi ya wabunge na watendaji wa serikali kwamba ni mafisadi, zilitokana na nongwa ya kukosa “Ufesti Ledi’ (kuwa mke wa rais). Mbali na Mzee Malecela na mkewe, Waziri Simba pia alimgeukia Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi akimtuhumu kuwa anaendesha vyombo vya habari vinavyoichafua CCM na serikali yake kwa maslahi binafsi. Pia alimshambulia Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, akiwatuhumu kuwa ni watu wenye njaa na kwamba wanalipwa fedha za kufanya kazi ya kupambana na ufisadi. Waziri Simba alisema hata tuhuma dhidi ya Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, zimetokana na chuki binafsi. Alisema uchunguzi wa kashfa ya rada ulishamalizika na Chenge akasafishwa na kuongeza kwamba, hata uchunguzi wa Richmond ulibaini kwamba hakukuwa na rushwa.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote