
Stacey Herald,Mama mwenye umbile dogo kuliko wote duniani amejifungua salama mtoto wa tatu pamoja na kwamba madaktari walimuonya kuwa angeweza kupoteza maisha yake kutokana na ukubwa wa tumbo lake ambalo lilimfanya ashindwe kutembea. Mama mwenye umbile dogo kuliko wote duniani ambaye ana urefu wa sentimeta 71 tu, amejifungua salama mtoto wa tatu wa kiume pamoja na kwamba kulikuwa na hofu ujauzito wake ungeweza kusababisha apoteze maisha.Stacey Herald, mkazi wa Kentucky nchini Marekani amejifungua mtoto wa kiume mwenye uzito wa kilo 1.2 ambaye amempa jina la Malachi.Stacey mwenye umri wa miaka 35, ana watoto wawili wa kike aliozaa na mumewe Will mwenye umri wa miaka 27.Stacey alipingana na ushauri wa madaktari kwa mara ya tatu ndani ya miaka mitatu kwa kuzaa watoto watatu ingawa madaktari walimuonya kuwa ujauzito ni hatari kwa afya yake.Mtoto wake watatu alizaliwa wiki iliyopita kabla ya muda wake akiwa na wiki 32 tu tumboni baada ya madaktari kuona kuwa kwa jinsi tumbo la Stacey lilivyozidi kuwa kubwa, viungo vyake vya ndani vingeweza kupasuka.Stacey ameruhusiwa kurudi nyumbani kwake ingawa mtoto wake ataendelea kubakia hospitali akipatiwa matibabu zaidi.Stacey anasumbuliwa na ugonjwa unaoitwa Osteogenesis Imperfecta, ambao husababisha mifupa kuwa dhaifu yenye kuvunjika kirahisi, mapafu dhoofu na ugonjwa huo umemsababishia asirefuke.Mumewe ana urefu wa mita 1.71 na watoto wao wawili hivi sasa wameisharefuka kuzidi urefu wa mama yao.Mtoto wake wa kwanza Kateri alizaliwa mwaka 2006 akiwa na urefu nusu ya urefu wa mama yake kwa bahati mbaya alirithi ugonjwa wa mama yake kwahiyo naye pia hatarefuka atakuwa kama mama yake.
No comments:
Post a Comment