Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Friday, December 11, 2009

Mashoga Uganda Kuhukumiwa Adhabu ya Kifo?

Wakati Marekani baadhi ya majimbo yanaruhusu ndoa za jinsia moja, Mashoga watakaokamatwa nchini Uganda watahukumiwa adhabu ya kifo na familia zao zitatupwa jela miaka saba iwapo zitashindwa kuwafichua hadharani huku wenye nyumba watakaowapingasha nyumba zao mashoga nao huenda wakanyea kwenye makopo ya jela. Hayo yamo katika muswada mpya wa sheria ya kupambana na ushoga nchini Uganda ambao uko njiani kupitishwa kuwa sheria.Muswada huo umezua mtafaruku katika jamii ya mashoga duniani na leo alhamisi maandamano ya mashoga wa Uingereza yanafanyika jijini London kuupinga muswada huo.Mwezi uliopita mashoga wa Marekani waliandamana kuupinga muswada huo ambao Uganda imesisitiza itaupitisha pamoja na shinikizo kubwa toka mataifa wafadhili.Watetezi wa haki za mashoga na wasagaji wamedai kuwa muswada huo utarudisha nyuma juhudi za kupambana kuzuia kuenea kwa ukimwi. David Cato(pichani), shoga ambaye aligeuka kuwa mtetezi wa mashoga baada ya kupewa kipigo mara nne, kutiwa mbaroni mara mbili na kufukuzwa kazi kwasababu ya ushoga wake, alisema: "Wakati tulipojitokeza kudai haki zetu ndio wameamua kutunga sheria dhidi yetu".Cato pamoja na wanaharakati wenzake wa kutetea haki za mashoga na wasagaji wanahofia muswada huo utapitishwa kuwa sheria. Hata hivyo baadhi ya raia wa Uganda wanauunga mkono muswada huo ili kukomesha tabia ya ushoga na usagaji ambayo imekuwa ikukua kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni."Vijana wa sekondari wanaiga kila kitu toka nchi za kimagharibi na Marekani", alisema mwalimu wa sekondari David Kisambira ambaye anaunga mkono muswada huo."Kuna idadi kubwa ya wanafunzi wamegeuka kuwa mashoga na wasagaji, tunasikia kuwa kuna vikundi vya watu vinavyopewa pesa na taasisi za mashoga katika nchi zilizoendelea, zinaajiri vijana na kuwaingiza katika shughuli za kishoga", alisema mwalimu huyo.Kisambira kama walivyo viongozi wengi wa Uganda wanataka sheria kali zitungwe ili kutokomeza suala hilo.

1 comment:

Anonymous said...

mbona hiyo kali sasa, dunia imefika mwisho sasa yani mpaka mashoga wanajitokeza hadharani????? bora wauliwe tu hao mashoga kwani ni aibu kwa tsifa zima.

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote