Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Friday, December 11, 2009

Apasua tumbo la mjamzito na kutaka kuiba kichanga

Mwanamke mmoja wa nchini Marekani ( pichani) ambaye alikuwa na ndoto ya kupata mtoto, amefunguliwa mashtaka ya kujaribu kuua baada ya kulipasua kwa kutumia kisu tumbo la mwanamke mjamzito akiwa na nia ya kuiba kichanga kilichokuwa tumboni mwake. Mwanamke mwenye umri wa miaka 40 aliyetambulishwa kwa jina la Veronica Deramous mkazi wa Maryland, Marekani aliwatangazia familia yake pamoja na mpenzi wake kuwa ana mimba na anatarajia mtoto hivi karibuni.Lakini ukweli ni kuwa Veronica hakuwa na mimba na alitiwa mbaroni akikabiliwa na mashtaka ya kujaribu kuua baada ya kulipasua tumbo la mwanamke mjamzito ili amuibie kichanga chake kilichokuwa tumboni.Taarifa ya polisi ilisema kuwa Veronica alitengeneza urafiki na mwanamke mjamzito aliyekuwa hana makazi akilala mitaani akimlaghai kuwa atampa makazi kwenye nyumba yake na atampa vyakula na nguo bure.Lakini mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 29 alipoingia nyumbani kwa Veronica, alifungwa mikono yake na kuwekwa mateka kwa siku tano.Taarifa ya polisi iliendelea kusema kuwa Veronica alijaribu kulipasua tumbo la mwanamke huyo ili kukiiba kichanga chake kilichokuwa tumboni.Hata hivyo mwanamke huyo alifanikiwa kutoroka kabla ya Veronica hajakamilisha azma yake baada ya Veronica kupitiwa na usingizi.Mwanamke huyo aliokolewa na polisi waliomkuta kwenye maegesho ya gari ya nyumba hiyo huku akivuja damu kwa wingi.Aliwahishwa hospitali ambako ilibidi azalishwe kwa njia ya upasuaji na mtoto wake wa kike alizaliwa salama akiwa na afya njema na ameamua kumpa jina la "Miujiza".Veronica anashikiliwa na polisi akikabiliwa na mashtaka ya kujaribu kuua na utekaji.

1 comment:

Anonymous said...

[url=http://www.ganar-dinero-ya.com][img]http://www.ganar-dinero-ya.com/ganardinero.jpg[/img][/url]
[b]Necesitas ganar dinero y no sabes que hacer[/b]
Nosotros hemos encontrado la mejor guia en internet de como ganar dinero. Como fue de utilidad a nosotros, tambien les puede ser de utilidad a ustedes. No son unicamente formas de ganar dinero con su pagina web, hay todo tipo de formas para ganar dinero en internet...
[b][url=http://www.ganar-dinero-ya.com][img]http://www.ganar-dinero-ya.com/dinero.jpg[/img][/url]Te recomendamos entrar a [url=http://www.ganar-dinero-ya.com/]Ganar-dinero-ya.com[/url][url=http://www.ganar-dinero-ya.com][img]http://www.ganar-dinero-ya.com/dinero.jpg[/img][/url][/b]

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote