Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, December 8, 2009

Chanzo cha Ajali SUKA KIMARA chajulikana!!!!!

DEREVA aliyesababisha ajali jana katika eneo la Kimara Suka na kusababisha vifo vya watu wawili papohapo chanzo kilichomfanya asababishe ajali hiyo yahisiwa. Hayo yalijulikana baada ya mwanamke mmoja aliyekuwa akilia kwa uchungu na kupiga kelele zisizo na mfano eneo la tukio huku akinukuliwa maneno na mashuhuda eneo la tukio.Mwanamke huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa hajui atafikaje kwao mkoani Mbeya baada ya mpenzi wake huyo kukamatwa na kupelekwa polisi.Alidai kuwa yeye na dereva huyo walikuwa wakielekea mkoani Mbeya ambapo dereva huyo alikuwa ni mwajiriwa wa kampuni ya Total.Alisema hajui ilikuwaje hadi kutokea ajali hiyo baada ya kulopoka kuwa usiku wa kuamkia safari hiyo walikesha kwenye hoteli moja jijini kwa ajili ya matanuzi na walichelewa sana kulala na asubuhi yake ndipo walipoanza safari hiyo.“ Sijui ilikuwa ni usingizi jamani sijui pombe zilikuwa hazijamtoka au …. Jamani ameshaua nitafanyaje mimi jamani nitafikaje Mbeya mimi? Alijiuliza huku akinukuliwa na baadhi ya watu eneo la tukio bila kujijuaHivyo baada ya kutoa siri hiyo baadhi ya watu kama unavyojua baadhi walianza kumshambulia kwa maneno na kumshutumu kuwa yeye ndiye aliyesababisha ajali hiyo.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote