Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Wednesday, December 16, 2009

Mtoto mdogo mwenye uwezo mkubwa wa kuogelea kuliko wote duniani

Mtoto Gibson Walker wa nchini Australia ana umri wa miezi 18 tu lakini ana uwezo wa kuogelea na kupiga raundi nne katika bwawa la kuogelea lenye urefu wa mita 25.Akifanya mazoezi katika kituo cha mazoezi ya kuogelea cha Gulliver Coomera Swim Centre, Gibson huogelea kwa mwendo kobe wa taratibu lakini hufanikiwa kumaliza raundi nne kuzunguka bwawa la kuogelea bila kupumzika.Baba yake Gibson, Mark alisema kuwa alianza kumfundisha mwanae kuogelea tangia alipokuwa na umri wa miezi sita na ghafla alianza kupenda kuogelea."Anajiamini sana anapoogelea kiasi cha kunifanya nisiwe na hofu yoyote", alisema baba wa mtoto huyo.Mafunzo ya kuogelea aliyopewa akiwa na umri mdogo yalimsaidia mtoto huyo kuokoa maisha yake wakati alipodondoka pembeni ya bwawa la kuogelea na kuangukia kichwa kabla ya kuangukia kwenye bwawa la kogelea.Gibson badala ya kuanza kulia kama watoto wenzake ambavyo wangefanya, aliogelea hadi kwenye ukingo wa bwawa hilo na kujitoa mwenyewe nje ya bwawa hilo ndipo akaanza kulia.Mwalimu wake wa kuogelea Terry Gulliver ana rekodi nzuri ya kuwafundisha watoto wenye umri mdogo kuogelea. Aliwahi kumfundisha mtoto wa miaka mitatu kuweza kuogelea mita 1500 bila matatizo yoyote."

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote