Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, December 7, 2009

Ashushiwa kipigo baada ya kufumaniwa na Mke wa Jirani

MWANAMME mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Hamisi [43] alijikuta akipata aibu ya mwaka baada ya kufumaniwa na mke wa jirani yake huko maeneo ya Manzese Tiptop eneo la Shidele. Mtoa taarifa wa tukio hilo ambaye ameombwa kutotajwa jina amesema kuwa mwanaume huyo alifumaniwa akiwa na mke wa rafiki yake huyo ambaye ni jirani wake wa karibu wa familia hiyo.Alidai kuwa mwenye mke ambaye alifahamika kwa jina la “Denda” alipata tetesi hizo na kuambiwa na baadhi ya watu kuwa mke wake alikuwa akichukuliwa na jamaa yake huyo na yeye kutokuamini kile ambacho alikuwa anaambiwa na watu hao.Usiku wa kuamkia jana, mwenye mke alishuhudia yeye mwenyewe baada ya kuweka mtego wa kumuaga mke wake hatorudi usiku huo.Hivyo katika hali ambayo alishindwa kuiamini mwanaume huyo alirudi nyumbani kwake hapo majira ya saa 6 za usiku na kukuta mke wake huyo hayupo na kuambiwa kuwa yupo nyumba ya pili kwa jamaa yake.Alifanya juhudi zote kuhakikisha kuwa anahakikisha maneno ya watu alikwenda kujibanza kwenye nyumba hiyo ya pili alipokuwa akiishi rafiki yake huyo ili aweze kumuona mke wake akitokea kwenye chumba cha jamaa yake huyo.Bila kutarajia kwenye majira ya saa 10:45 alfajiri alimuona jamaa yake akitoka nje kwenda kujisaidia kwa kuwa choo kilikuwa ni cha nje alieendeelea kubana, baada ya dakika kadhaa alimuona mke wake nae akitoka nje kwenda kujisaidia akitokea kwenye chumba cha jamaa yake huyo.Alimuangalia mke wake huyo na kuhakiki akirudi tena kwenye chumba cha jamaa huyo, ndipo alipokwenda kutoa taarifa kwa jamaa zake wachache ili waweze kushuhudia tukio hilo. Mashuhuda walipofika kwenye chumba hicho waligonga mlango walipoona haufunguliwi walichukua uamuzi wa kuvunja mlango na kuwakuta wapendao hao wakiendelea na shughuli zao kama kawaida.Aibu kubwa ilimpata baba huyo na mke huyo hali kadhalika na watu walishafurika eneo hilo kushuhudia jamaa huyo alivyomsaliti rafiki yake huyo kwa kumchukulia mke wake.Bila kuchelewa wenye hasira kali walianza kumpiga na kumshambulia hadi kupelekea kujeruhiwa maeneo yake ya usoni.Hivyo watu walimwambia “leo kwa vile umeona mwenyewe basi uamuzi ni wako tulikuwa tunasubiri uone mwenyewe tulikuwa tunakwambia muda marefu ulikuwa hutuamini”Bila kuchelewa mwenye mke aliingia ndani na kutoka na karatasi mkononi yaani aliandika talaka na mke huyo kutakiwa kuondoka kuingia ndani kwake na kuchungua nguo zake na aondoke kwao.Bila kutarajia mwanamke huyo alikwenda kuchukua nguo zake na kurudi tena kwa jamaa aliyefumaniwa nae na kuwaaacha wakazi wa maeneo kubaki wakimshangaa mwanamke huyo kwa kitendo chake hicho cha kutoka chumba kimoja kuhamia kingine.HAta hivyo ilidaiwa na chanzo hiki kuwa Saidi ambaye alifumaniwa alimwambia mtoa taarifa hii kuwa “ Mimi sio mchezo mwanamke mwenyewe amehama kwake amekuja kwangu”“ Halafu hatujaanza mahusiano leo, yule mwanamke mchana huwa kwangu jioni anarudi kwa mume wake” anasema

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote