Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, December 14, 2009

Secretary wa Ubalozi aliwatemea Mate Polisi na Muandishi wa Habari arudishwa kwao!!!

OFISA wa Ubalozi wa Canada nchini, Jean Touchatte (48) aliyemtemea mate askari wa usalama barabarani na mwandishi wa habari kwa nyakati tofauti, amerudishwa nchini kwao. Touchatte aliwatemea mate watumishi hao wa umma Jumatano iliyopita, Dar es Salaam. Ubalozi wa Canada umemuamuru aondoke mara moja, na nchi hiyo imeeleza kusikitishwa na kitendo hicho. Taarifa ya ubalozi iliyotolewa jana Dar es Salaam, imesema, “tunasikitika kwa tukio la Jumatano, Desemba 9 likihusisha mmoja wa maofisa wetu.”Touchatte alikuwa Katibu Muhtasi wa ubalozi. Ubalozi huo umesema, kwa faida ya pande zote, umeona ni vyema ofisa huyo aondoke mara moja na arudi Canada. Touchatte alimtemea mate Koplo Samson na baadaye akafanya hivyo kwa Mwandishi wa habari, Jerry Muro (29) wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Muro amesema, hakubaliani na hatua ya ubalozi kumwondoa nchini kabla ya kufikishwa katika vyombo vya sheria. Amesema, ataendelea kufuatilia ili kuhakikisha kwamba mtuhumiwa huyo anaadhibiwa kisheria. “Sikubaliani. Lazima haki itendeke. Kumfukuza ni hatua mojawawapo, lakini haimaanishi kwamba yamekwisha. Nitakwenda polisi wazuie hati yake ya kusafiri,” amesema Muro.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote