Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, December 21, 2009

Ndoa ya Wazazi wa BEYONCE yavunjika!!!!!!!!!!

Mama yake Beyonce, Tina Knowles, amefungua madai ya talaka mahakamani kuivunja ndoa yake na mumewe Mathew Knowles iliyodumu miaka 29.Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana Tina alifungua jalada la madai ya talaka kwenye mahakama moja ya Texas mwezi uliopita huku tetesi zikisema kuwa sababu ya kuvunjika kwa ndoa hiyo ni mumewe kutokuwa muaminifu na kuisaliti ndoa yao.Mathew amekuwa akitajwa sana kwenye vyombo vya habari kwa miaka kadhaa kuwa anatembea nje ya ndoa yake na hivi karibuni alifunguliwa kesi na mwanamke mmoja wa Los Angeles akituhumiwa kumpa mimba na kumtelekeza.Tina na Mathew walifunga ndoa mwaka 1980 na walizaa watoto wawili Beyonce na Solange. Wana mjukuu mmoja mwenye umri wa miaka 5.Mathew ndiye meneja wa shughuli za muziki za binti yake Beyonce wakati Tina anasimamia duka lake la nguo linaloitwa "House of Deréon" alilofungua na Beyonce mwaka 2006.Mwezi juni mwaka huu, jarida moja la udaku la Marekani liliripoti kuwa shughuli za kimuziki na biashara zimewafanya wazazi wake Beyonce waishi mbali mbali kwa muda mrefu.Beyonce akiongea katika mahojiano na jarida la Giant mwaka jana alisema kuwa amejifunza mengi kutokana na ndoa ya wazazi wake.Beyonce ambaye alifunga ndoa na rapa milionea Jay-Z mwezi aprili mwaka jana alisema kuwa amejifunza kuwa maisha ya ndoa si lelemama, wazazi wake wamekuwa wakikorofishana na kupatana mara kwa mara na kuna wakati waliishi pamoja wakati mwingine wakiishi tofauti.Mdogo wake Beyonce, Solange mwenye umri wa miaka 23, aliolewa wakati alipokuwa na umri wa miaka 17 na mchezaji soka Daniel Smith, lakini ndoa yao haikudumu sana na ilivunjika mwaka 2007.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote