Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, December 17, 2009

Phiri wa Simba kutua leo

KOCHA wa Simba, Patrick Phiri anatarajiwa kutua nchini leo akiwa na matumaini ya kuchukua ubingwa wa michuano ya Tusker iliyoanza kutimua vumbi jana kwenye Uwanja wa Uhuru. Afisa habari wa Simba, Clifford Ndimbo alisema kuwa pamoja na kuchelewa kuja kuinoa timu hiyo kocha huyo bado ana imani kubwa na kikosi chake kufanya vizuri katika michuano hiyo.'' Ni kweli kocha amechelewa kuja baada ya kwenda likizo fupi ya ligi kuu Tanzania Bara, lakini yeye anakijua kikosi chake na anajua kuwa akiwafundisha kwa siku ngapi wanaweza kufanya vizuri hiyo ni kazi yake mwenyewe siwezi kumsemea,'' alisema Ndimbo.Aliongeza kuwa kikosi chao kimetua Dar es Salaam jana kikitokea Zanzibar walipokwenda kuweka kambi ya siku tano wakiwa chini ya kocha msaidizi Amri Said na wamejiandaa vizuri katika michuano hiyo.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote