Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, December 15, 2009

Kesi ya akina Mramba kusikilizwa siku 3 mfululizo

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, leo itaendelea kumsikiliza shahidi wa tatu kwenye kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7 inayowakabili mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba, Daniel Yona na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja. Kesi hiyo inasikilizwa na jopo la mahakimu watatu wakiongozwa na Mwenyekiti John Utamwa, Saul Kinemela na Sam Rumanyika, itasikilizwa kwa mfululizo hadi Desemba 18, mwaka huu. Awali, mahakama hiyo ilisikiliza mashahidi wawili na iliahirishwa hadi shahidi wa tatu atakapotoa ushahidi wake. Katika kesi hiyo, washtakiwa wanadaiwa kuwa kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14, mwaka 2004, jijini Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kama mawaziri na katibu mkuu walitumia vibaya madaraka. Ilidaiwa kuwa kwa kupitia kampuni ya Alex Stewart (Assayers) ya Uingereza iliyoingia mkataba wa ukaguzi wa madini kupitia kampuni tanzu ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation waliingia mkataba kukagua kiwango cha uzalishaji wa madini ya dhahabu kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma. Awali shahidi wa kwanza Nyelo Godwin (48) alidai mahakamani hapo kwamba mkataba wa kampuni ya Alex Stewart ulipitishwa licha kuwepo kwa mapendekezo ya kuuzuia usisainiwe. Pia, alidai kuwa kati ya asilimia 3 ya fedha zilizokuwa zinapatikana kwa mwaka, kampuni hiyo ilikuwa inalipwa asilimia 1.9 na serikali ilibaki na asilimia 1.1. Naye shahidi wa pili, Betha Soka (44) alidai kwamba Yona alimdanganya Rais wa awamu ya tatu kwa kumpelekea taarifa kwamba majadiliano ya mchakato wa kuipa kazi ya ukaguzi wa madini Kampuni ya Alex Stewart yalishirikisha ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Soka alidai kupitia dokezo lililoandikwa na mshitakiwa wa pili Yona, kwamba majadiliano ya mchakato huo yalifanywa kwa pamoja kwa kuhusisha wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha, Benki Kuu Tanzania (BoT) na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na alimjulisha Rais Mkapa kuwa yanaendelea vizuri.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote