Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, December 7, 2009

Umaga Afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo

MCHEZA mieleka 'Umaga' Eki Eddie Fatu amefariki nyumbani kwake huko Houston kwa ugonjwa wa moyo. Umaga mwenye miaka 36, alikutwa chumbani hajitambui na mkewe ambaye alimkimbiza hospitali, ambako alipata tena mshtuko wa moyo kwa mara ya pili kabla hajafariki. Umaga ambaye anafahamika kwa michoro ya tatoo aliyojichora mwilini, pia anafahamika sana kwa sababu ya familia aliyotokea ambayo ni mashuhuri kwa mchezo wa mieleka. Fatu au Umaga, umaarufu wake ulijitokeza zaidi mwaka 2007 alipofanya vizuri katika mashindano ya Wrestlemania. Hivi karibuni Umaga alikuwa nchini Australia akitangaza mchezo wa mieleka. "Kwa niaba ya familia ya Anoii na Fatu, tumesikitishwa sana na kustuka kumpoteza Eki," Afa Anoii alisema. Alisema,"familia yetu kiujumla tumeumia sana moyoni na maneno hayawezi kelezea kila mmoja wetu anavyojisikia, lakini tumefarijika kufahamu mpendwa wetu alikuwa akipendwa sana na familia yake, marafiki zake, watu aliokuwa nao na mashabiki wake kiujumla." Umaga anatokea familia ya wacheza mieleka ya Samoan ambayo inafahamika kwa sababu ya kukuza biashara ya mchezo wa mieleka, tangu enzi za mjomba wake, kaka zake Afa na Sika Anoiia ambao walifahamika kama 'The wild Samoans' katika miaka ya 1970 na 80, pia yupo binamu yake aitwaye Dwayne 'The Rock Johnson' ambaye aliacha kucheza mieleka na hivi sasa ni muigizaji Hollywood.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote