Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, December 31, 2009

Ataka kuua baada ya kunyimwa Penzi kinyume na Maumbile

OMARI Mohamed (22), mkazi wa Yombo jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke kujibu, shtaka la kutaka kumuua msichana baada ya kukataa kumwingilia kinyume na maumbile. Akisoma hati ya mashitaka, Inspekta Isaya Mwanga mbele ya Hakimu Aziza Kalili wa mahakama hiyo alidai kuwa,mshitakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 10, mwaka huu katika majira ya saaa 2 usiku huko Yombo Kilakala. Alidai baada ya mshitakiwa kumwambia mlalamikaji kuwa alikuwa anahitaji kumwingilia kinyume na maumbile mlalamikaji alikataa kufanyiwa kitendo hicho na ndipo Omari alimchoma kisu cha tumbo, mgongoni na kwenye ubavu jambo ambalo lilimsababishia kuzirai na kupoteza fahamu papohapo. Alidai hali hiyo ilimfanya mlalamikaji apoteze fahamu papohapo na kukimbizwana wasamaria wema katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi. Mlalamikaji baada ya siku mbili aliweza kupata fahamuna kueleza umma jinsi ilivyokuwa na mshitakiwa kwenda kukamatwa Hata hivyo mshtakiwa alipotakiwa kujibu shtaka hilo, alikana na alipelekwa rumande kwa kukosa dhamana, na kesi imeahirishwa hadi Januari 7, mwaka huu itakapotajwa tena.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote