Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Wednesday, December 16, 2009

Dunia Imeisha - Mtawa Kortin kwa Utapeli!!!!!

MTAWA wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Angela Singira (pichani), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka matano tofauti ya kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu. Kesi hizo zilisomwa jana mahakamani hapo na waendesha mashtaka mbalimbali mbele ya mahakimu wakazi wanne tofauti. Mwendesha mashtaka wa polisi Inspekta Boniface Edwin alimwambia Hakimu Ferdinand Kiwonde katika hati ya kwanza ya mashtaka kuwa, kati ya Aprili 10 na 20 mwaka huu, saa 3:00 asubuhi maeneo ya Bunju 'A', jijini Dar es Salaam, mtuhumiwa alijipatia mkopo wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh 625,000 kwa njia ya udanganyifu. Alisema mtuhumiwa huyo alijipatia mkopo huo kutoka kwa Isaya Rafael baada ya kujifanya wakala wa shule ya Sekondari ya Cornelius. Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huyo baada ya kujitambulisha hivyo, alichukua mboga za majani na viungo akieleza kuwa anawapelekea wanafunzi wa shule hiyo. Katika kesi ya pili, mtuhumiwa huyo anakabiliwa na shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Mwendesha mashtaka wa polisi Mohamed Kilongo alimwambia Hakimu Jackline Rugemalila kuwa Agosti 9 mwaka huu, saa 3:00 asubuhi maeneo ya Kinondoni, mtuhumiwa alijipatia Sh 250, 000 kutoka kwa Joackim Peter. Aliieleza mahakama kuwa katika shtaka la tatu mtuhumiwa huyo anakabiliwa na kesi ya kujipatia mkopo kwa kutumia nguvu. Kilongo alimwambia tena Hakimu Rugemalila kuwa Februari 5 mwaka huu saa 4:00 asubuhi maeneo ya Tegeta Machinjioni, mtuhumiwa alijifanya wakala wa Shule ya Sekondari ya Cornelius na kujipatia mkopo wa vitu vyenye thamani ya Sh 480, 000. Alisema baada ya utambulisho huo, alichukua kilo100 za mchele, maharage kilo 100, sukari kilo 25, unga wa mahindi kilo 50 na mikate 200 kutoka kwa Hassan Mahmud. Katika shtaka lingine mwendesha mashtaka huyo alisema bila kutaja jina lake la kwanza, Januari Mosi mwaka huu saa 5:00 asubuhi maeneo ya Salasala, jijini Dar es Salaam mtuhumiwa alijifanya wakala wa shule hiyo na kujipatia mkopo wa kilo 90 za maharage zenye thamani ya Sh117,000 kutoka kwa Christopher Bondi. Hati ya mashtaka pia imeeleza kuwa katika kesi ya tano mtuhumiwa huyo alijipatia mkopo wa vitu vyenye thamani ya Sh380,000 kwa njia ya udanganyifu. Mwendesha mashtaka wa polisi Inspekta Idd Kiwogoma alimwambia Hakimu Sundi Fimbo kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo baada ya kujifanya wakala wa shule hiyo ya sekondari na kuchukua mikate 130 kutoka kwa Haruna Issa. Hata hivyo, mtuhumiwa huyo alikana mashtaka hayo yote na kesi hiyo kuahirishwa hadi Desemba 29, mwaka huu itakapotajwa tena. Dhamana ya mtawa huyo ilikuwa wazi, lakini hakupata mdhamini hivyo alipelekwa rumande.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote