Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, December 17, 2009

Mwanamke afia nyumba ya wageni Kimara

MWANAMKE ambaye hakuweza kufahamika jina wala makazi yake anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 na 30, amekutwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Marangu huko Kimara jijini Dar es salaam. Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, amesema tukio hilo limetokea huko maeneo ya Kimara Mwisho.Alisema maiti ya mwanamke huyo ilikutwa ikiwa imelala kitandani huku mdomoni ikiwa inatoka mapovu na haikuweza kufahamika mara moja chanzo cha kifo hicho.Alisema kuwa, mwanamke huyo alifika katika gesti hiyo Desemba 13, majira ya saa 4 asubuhi na alipanga katika nyumba hiyo akiwa na kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la James Joshua, mkazi wa jijini Dar es Salaam.Katika maelezo yaliyopatikana katika nyumba hiyo ilidaiwa kuwa, kwa mara ya mwisho mwanamume huyo aliaga kwa mhudumu mmoja aliyekuwa zamu kuwa anakwenda kutafuta chakula aina ya chipsi na hakurejea tena.Amesema baada ya wahudumu kutaka kuingia katika chumba hicho kwa nia ya kufanya usafi, ndipo walipobaini dada huyo kuwa alikuwa ameshakufa.Maiti imehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala na polisi wanaendelea kumsaka kijana huyo kwa udi na uvumba.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote