Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, December 21, 2009

Mahabusu watoroka chini ya Ulinzi wa POLISI!!!!!!!!!!!!

Mahabusu watatu wanadaiwa kutoroka chini ya ulinzi wa askari wa Jeshi la Polisi wakati wakisafirishwa kutoka Mahakama ya Mwanzo Nata kwenda Gereza la Wilaya ya Serengeti la Mugumu. Mahabusu hao walitoroka Ijumaa iliyopita majira ya saa 9:30 alasiri wakati wakisafirishwa kwa basi baada ya kufika eneo la mto Rubana likielekea mjini Serengeti. Baada ya kufika eneo hilo, basi hilo lilinusurika kupinduka kutokana na barabara kuharibika vibaya na kusababisha abiria akiwamo askari huyo kuruka ili kunusuru maisha yao. Baada ya kuteremka, inadaiwa kuwa askari huyo alijisahau hali iliyowapa nafasi mahabusu hao kutoroka na kwenda kusikojulikana na kubakia na maabusu mmoja. Hata hivyo Kamanda Polisi Mkoa wa Mara, Boaz Robert, aliliambia Nipashe kuwa mahabusu waliotoroka ni wawili na mmoja alibaki mikononi mwa askari huyo. “Tuko hilo lilitokea Ijumaa saa kumi kasorobo baada ya basi waliokuwa wamepanda kupata misukosuko ... watuhumiwa hao walitoroka wakipelekwa kwenye gereza la Mugumu, walipata nafasi ya kutoroka baada ya basi hilo la AM kunusurika kupinduka hivyo kila mmoja akawa anatoka kujinusuru, ” alisema Kamada Boazi Aliwataja mahabusu walotoroka kuwa ni Thomas Kemncha (30) ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa kosa la shambulio na Gitati Gisemwe (20), mkazi wa Nata aliyekuwa anatuhumiwa kwa wizi. Boazi, alisema mahabusi Ndalahwa Tulami (32), mkazi wa Isenye ambaye anatuhumiwa kwa kuchoma nyumba alibaki mikononi mwa polisi na kwamba waliotoroka wanaendelea kusakwa na jeshi hilo

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote