Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Friday, December 18, 2009

Ajali mbaya yatokea SAME watu 30 wahofiwa kufa

WATU zaidi ya 30 wanahofiwa kufa katika ajali nyingine mbaya iliyohusisha basi la kampuni ya Mohamed Trans ambalo liligongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Asia Combi lililotokea eneo la Kandoto, nje kidogo ya mji wa Same mkoani Kilimanjaro. Basi hilo lenye namba za usajili T 810 AQM na ambalo lilikuwa likitokea Nairobi kwenda Dar es salaam, lililigonga basi hilo dogo ambalo inasemekana lilibeba ndugu waliokuwa wakienda Marangu kwenye harusi. Hii ni mara ya tatu katika kipindi cha miaka mitatu kwa mabasi ya kampuni ya Mohamed Trans kupata ajali mbaya iliyochukua maisha ya watu wengi, baada ya ajali iliyochukua uhai wa watu 30 mwezi Juni mwaka 2007, na ile ya Julai mwaka huu iliyotokea Korogwe, Tanga na kuchukua roho za watu 25. Hadi saa 1:00 usiku idadi ya abiria waliothibitishwa kufariki dunia ilikuwa watu 19 na karibu wote ni wale waliokuwa kwenye basi dogo aina ya Asia Combi lenye namba za usajili T 845 BCD lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Moshi. Mganga mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Same, Dk Charles Kifunda aliithibitishia gazeti moja kuwa hadi saa 1: 00 usiku abiria 19 walikuwa wamethibitishwa kufariki ingawa taarifa nyingine zilidai kulikuwa na maiti 28 chumba cha maiti. Hata hivyo alisema kwa wakati huo haikuwa rahisi kutambua waliopoteza maisha. Basi la Asia Combi linafanya safari za daladala kati ya Sinza na Tandika jijini Dar es Salaam. Ajali hiyo ilitokea saa 10:00 jioni katika eneo la Kandoto nje kidogo ya mji wa Same mkoani Kilimanjaro katika barabara kuu ya Moshi-Dar es Salaam, eneo ambalo si hatari kwa ajali kama ilivyo maeneo mengine. Hali ilikuwa ya kutisha kwenye eneo la ajali kutokana na viungo vya watu, ikiwa ni pamoja na vichwa, miguu, mikono na ubongo kuzagaa pamoja na damu nyingi huku kukiwa na vilio kutoka kwa abiria waliojeruhiwa na wananchi ambao walikuwa wakishuhudia maiti na majeruhi hao.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote