Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, December 17, 2009

Ama kweli Mjini shule! unajua maana halisi ya Machinga? pata uhondo

Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni! eti kuna tetesi kuwa hili neno la Wamachinga watu wanalielewa vibaya wabongo wengi wanafikiri kuwa wamachinga ni wale wafanyabiashara za mkononi hasahasa watu wanaotoka mikoa ya kusini, lakini ukweli ni kwamba biashara hizi hazifanywi na watu wanaotoka kusini tu ila watu wanaotoka mikoa mbalimbali katika nchi yetu

Wamachinga ni kabila mojawapo linalopatikana katika Mkoa wa lindi na jamii hii inapatikana katika maeneo ya Mchinga, mila na desturi za kabila hili hazina tofauti na watu wengine wanaotoka mikoa ya pwani.

Wabongo wengi wamelielewa Neno hili vibaya lakini kutokana na tembeatembea yangu mtaani inaonyesha walikuwa wanamaanisha (Maching - Guy) yaani wanafanyabiashara wanaofanya biashara za kutembea toka sehemu moja kwenda nyingine sasa wao baada ya kutamka Maching - Guy wanatamka Machinga ndio hapo watu wakaanza kusambaza uvumi huu na kusema wanaofanya biashar hizi ni watu kutoka kusini .


1 comment:

Godwin Habib Meghji said...

Hii nimeipenda, Sikuwahi kufikiria hili. Nilikuwa najua tu ya kariakoo

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote