Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, December 7, 2009

Amuambukiza Mkewe HIV kwa Makusudi

Mwanaume mwenye maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, amemuambukiza mkewe aliyekuwa amelala ugonjwa huo baada ya kumchoma na sindano ya kushonea nguo aliyopakaza damu yake yenye virusi hivyo.Inaaminika kuwa mwanaume huyo alichukua uamuzi huo wa kumuambukiza mkewe ukimwi ili mkewe akubali kufanya naye mapenzi, limeripoti gazeti moja la nchini New Zealand.Hilo ni tukio la kwanza kutokea nchini New Zealand kawaida watu huambukiza wenzao ukimwi kwa kufanya mapenzi bila kutumia kinga.Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 35 amekiri kumuambukiza ukimwi mkewe mwenye umri wa miaka 33 na ametupwa rumande akisubiri hukumu ya kumuambukiza mtu makusudi ugonjwa huo. Huenda akahukumiwa kutumikia kifungo jela cha miaka 14.Jina la mwanaume huyo na mkewe hayakutolewa kwa sababu za kisheria.Mwanaume huyo aligundulika ana ukimwi wakati alipofanyiwa uchunguzi wa afya yake wakati wa yeye na familia yake walipowasili nchini New Zealand mwaka 2004.Hata hivyo mkewe na watoto wake hawakugundulika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo. Mkewe aliamua kuendeleza uhusiano wao ili watoto wao wasipate shida kutokana na kutengana kwao lakini aligoma kufanya naye mapenzi.Mwanamke huyo alielezea jinsi alivyoamka asubuhi mwezi mei mwaka jana na kukuta alama ya sindano kwenye paja lake la mguu wa kushoto. Siku hiyo hiyo alishangaa kumkuta mumewe akiwa chumbani kwao huku akiwa ameshikilia sindano ya hospitali ikiwa imejaa damu.Siku mbili baadae aliamka tena asubuhi na kukuta alama ya sindano kwenye mguu wake. Mumewe alikanusha kumdunga sindano lakini aligundua ushahidi wa damu kwenye blanketi lao.Mwezi septemba wakati daktari wake alipompima afya yake aligundulika ameambukizwa virusi vya ukimwi.Polisi walimfungulia mashtaka mumewe mwezi oktoba mwaka jana.Mwanamke huyo alisema kuwa ndoa yao ilikuwa na migogoro ya muda mrefu kutokana na yeye kugoma kufanya mapenzi na mumewe kwa kuhofia ataambukizwa virusi vya HIV.Baada ya kumbana sana kuhusiana na alama za sindano kwenye miguu yake, mwanaume huyo alikiri kutumia sindano ya kushonea nguo aliyoizamisha kwenye damu yake, kumchoma nayo mkewe ili amuambikize virusi vya ukimwi.Kitu alichokuwa akisema ni kuniomba radhi huku akisema "Nilitumia sindano kukuchoma nayo kwasababu nilitaka na wewe uwe kama mimi ili tuishi pamoja usinikimbie".

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote