Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, December 1, 2009

Habari njema kwa Wafungwa

WAFUNGWA wenye sifa ya kujiunga na elimu ya Juu, sasa watasomeshwa bure kupitia mfumo wa elimu masafa. Hatua hiyo, imefikiwa baada ya makubaliano maalum kati ya Wizara ya mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Magereza na Chuo Kikuu Huria Tanzania (CKHT). akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Makamu Mkuu wa CKHT Profesa Tolly Mbwette alisema makubaliano hayo yamekusudiwa katika mambo matatu, ikiwemo kuwapatia wafungwa taaluma na ujuzi ili waweze kurekebisha tabia na kuwapatia stadi za kuwawezesha kupambana na maisha baada ya kumaliza kutumikia vifungo vyao. Malengo mengine ya kuwapa elimu hiyo bure ni kushirikiana na Magereza katika kurekebisha tabia za wafungwa pamoja na kuwawezesha kutumia muda wao kwa manufaa yao wawapo gerezani, alisema Profesa Mbwette. Profesa Mbwette alifafanua kwamba katika makubaliano hayo, CKHT itamdahili mfungwa baada ya Jeshi la Magereza kuridhika na tabia yake na baada ya kutumikia kifungo kwa muda fulani. Pamoja na hayo, mfungwa huyo lazima aonyeshe tabia na mwenendo mzuri, alisema. Profesa Mbwette alisema pamoja na mambo mengine kwa sasa mfungwa atakayeomba na kukubaliwa kujiunga na CKHT, atahamishiwa kwenye gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam. Gereza la Ukonga, ni kama kituo cha Mkoa cha CKHT katika magereza ya Tanzania. Akiwa hapo mfungwa atapewa huduma zote za kitaaluma kama mafunzo ya muda mfupi, ya ana kwa ana gerezani, mitihani, majaribio na utafiti kwa mwanafunzi huyo,alisema. Alisema katika kuboresha huduma kwa wafungwa, CKHT kwa kushirikina na Book Aid International (Uk) na Jeshi la Magereza wamepanga kujenga maktaba ndogo ya kisasa. Katika maktaba, tutaweka samani ya vitu kama kompyuta na vitabu ndani ya gereza la Ukonga ili kuwawezesha wafungwa wengi zaidi pamoja na baadhi ya askari wanaosoma chuoni, kutumia huduma hiyo ili kujiendeleza kielimu katika muda mfupi ujao,alisema. Profesa Mbwette alisema CKHT ikishirikiana na Magereza wanampango wa kuwatembelea wafungwa na askari magereza kwenye magereza yote nchini ili kuwahamasisha kujiunga na CKHT. Mpango huu utafanyika kupitia kwa wakurugenzi wa vituo vya mkoa, kamati za ushauri za mikoa(RACs) na wakuu wa magereza husika, alisema Profesa Mbwette. Katika hatua nyingine, mfungwa Semayonga Ernest ,30, leo anatunukiwa shahada ya kwanza ya sheria na Chuo Kikuu Huria Tanzania(CKHT). Akizungumza jana Kamishna Mkuu wa Magereza Augustino Nanyoro alisema hatua hiyo ni matokeo ya urekebishaji wa tabia za wahalifu yanayofanywa na Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini. Hili ni tukio la pili, baada ya mfungwa Haruna Pembe Gombela kutunukiwa shahada kama hii Oktoba 31, 2007. Mafanikio haya ni matokeo ya urekebishaji wa wahalifu yanayofanywa na Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini,alisema Kamishna Nanyaro. Kamishna Nanyaro alifafua dhana ya urekebishaji wa wahalifu, inajumuisha program mbalimbali ambazo zinaandaliwa kwa ajili ya wafungwa ili kuwawezesha kubadili tabia ya uhalifu na kurejea kwenye jamii wakiwa raia wema. Kamishna huyo, alisema mfungwa Ernest alipata nafasi ya kusoma mara baada ya kurejeshwa nchini akitokea Mauritius alikokuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 10. Alianza kifungo Desemba 5, 2002 nchini humo. Lakini kutokana na utaratibu wa kubadilisha wafungwa, Desemba 28,2005, Ernest na wenzake walirejeshwa nchini na anatarajiwa kufunguliwa Agosti 10,2010. Mahafali ya Ernest yalifanyika jana katika viwanja vya kikosi Maalum Ukonga.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote