Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, December 15, 2009

Papic akiri kikosi cha Yanga bado ni dhaifu kinahitaji marekebisho

Kocha wa Yanga, Kostadin Papic amesema kuwa kikosi chake bado ni dhaifu na anahitaji kukifanyia marekebisho ya haraka kabla ya kuanza harakati za kuwania Kombe Tusker inayotarajiwa kuanza leo, jijini Dar es Salaam. Yanga inatarajia kuanza mshike mshike wa kuwania ubingwa wa michuano hiyo Ijumaa kwa kumenyana na Mafunzo ya Zanzibar. akizungumza na vyombo vya habari jana, Papic alisema kuwa hajaridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu yake kwenye mchezo wao wa kirafiki dhidi ya TMK United, ambapo mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini walikubali kipigo cha magoli 2-0. Papic alieleza kuwa mchezo dhidi ya TMK ulimsaidia kuona udhaifu wa timu yake, ambapo ili kuhakikisha wanatoa ushindani kwenye michuano hiyo wanahitaji mabadiliko ya haraka kabla ya kuingia uwanjani. "Nimeona timu yangu bado ni dhaifu, licha ya kwamba nyota wetu tisa walikuwa hawajarudi (kutoka kuziwakilisha timu zao za taifa katika michuano ya Chalenji nchini Kenya), na inahitaji marekebisho ya haraka ili kuhakikisha tunashindana kwenye michuano ya Tusker, sitaki tuwe washiriki, nataka tuwe washindani," alisema Papic. Aliongeza kuwa anaamini mabadiliko hayo yatafanyika mara baada ya wachezaji wake wote kurejea kwenye timu mara baada ya kumaliza majukumu ya timu zao za Taifa. Aliweka wazi kuwa timu kuwakosa zaidi ya wachezaji sita ni pengo kubwa ambalo linaweza kuiathiri timu kama ilivyotokea kwenye mchezo wao dhidi ya TMK. Papic aliongeza kuwa udhaifu mkubwa aliouona kwenye timu yake ni safu ya ulinzi ambayo imekosa kuelewana pale tu timu inaposhambuliwa huku washambuliaji wake wakishindwa kulijua jukumu lao wanapokuwa na mpira.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote