Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, December 7, 2009

Ajali Mbaya yatokea KIMARA SUKA Wawili wafa mmoja ajeruhiwa

Tukio hilo la kusikitisha limetokea asubuhi hii, majira ya saa mbili, katika eneo la Kimara Suka, baada ya mafundi 3 kukanyagwa na matairi baada ya lori lingine kusukumiza lori ambalo walikuwa wakitengeneza wao.Mafundi hao walikuwa wakitengeneza gari aina ya lori lililokuwa na namba za usajili T.427 AGX aina ya Scania ambalo liliharibika tokea juzi usiku eneo hilo ambalo walikuwa wakielekea mjini Arusha.Juhudi za mafundi hao jana kutwa nzima ziligonga mwamba baada ya kushindikana kuondoa lori hilo ambapo juhudi za mafundi hao zilitarajiwa kuzaa matunda asubuhi hii kwa kuwa katika hatua za mwisho katika kuondoa gari hilo ambalo liliharibika eneo hilo.Ilidaiwa kuwa mafundi hao watatu asubuhi hii walikuwa katika hatua za mwisho ambapo walishafanikiwa kukamilisha kitu ambacho kilikuwa kinakorofisha kwa siku mbili hizo.Hivyo bila kutarajia mafundi hao wkati wapo chini ya uvungu wa gari kukamilisha gari hilo kwa ajili ya kuanza safari, papohapo lilitokea lori jingine nyuma na kugonga lori hilo kwa nyuma na kuwasaga mafundi hao ambao walikuwa wakitengeneza lori hilo.Lori hilo lilisukumizwa kwa mbele na kufanya mafundi hao mmoja kusagwa kichwa na mwingine akiwa katika juhudi za kijitetea alichelewa na kusagwa na tairi maeneo yake ya kiuno.Mmoja kati ya mafundi hao alikuwa upande mwingine na alibahatika kuruka na kuacha mafundi wenzake wawili kufariki papohapo.Ilidaiwa kuwa baada ya kusababisha ajali hiyo dereva wa lori ambalo lilisababisha ajali ambaye hakuonyesha ushirikiano kwa kukataa kutaja jina lake alikuwa anajaribu kutaka kukimbia na wananchi wakamuwahi na kubaki hapo ambalo lori hilo lilikuwa na namba T 282 ADH aina ya Scania.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote