Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, December 3, 2009

Mtenda nae katendwa!!!!

Mtangazaji wa televisheni ya Iraq ambaye alitupwa jela miaka miwili kwa kumrushia viatu vyake rais wa zamani wa Marekani, George Bush, amekumbana na balaa kama hilo baada ya yeye naye kurushiwa viatu na raia wa Iraq nchini Ufaransa. "Umeiba staili yangu", alipiga kelele Muntadar al-Zaidi baada ya kukoswa koswa na kitu kilichoenda kugonga ukuta nyuma yake baada ya kukikwepa. Zaidi alijipatia umaarufu katika nchi za Kiarabu baada ya kumkosa kosa na viatu rais wa zamani wa Iraq, George W Bush.Bush alifanikiwa kuvikwepa viatu hivyo saizi namba 10 huku Zaidi akikamatwa hapo hapo na kutupwa mahabusu. Muntadar al-Zaidi alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kutokana na kitendo chake hicho alichokifanya wakati Bush alipowahutubia waandishi wa habari nchini Iraq.Zaidi alitolewa jela miezi michache iliyopita baada ya kifungo chake kupunguzwa.Akiongea na waandishi wa habari jijini Paris, Ufaransa kuhusiana na wahanga wa vita vya Iraq, Al Zaidi alikumbana na tukio kama alilomfanyia Bush. Raia mmoja wa Iraq aliyekuwa kwenye mkutano huo anayeziungana mkono siasa za Marekani huku akimlaumu Al Zaidi kwa kulinda udikteta nchini Iraq, alijitokeza na kumrushia kiatu chake Zaidi.kuonyesha kuwa damu ni nzito kuliko maji kaka yake Zaidi, Maithan aliyekuwepo kwenye kikao hicho, alimkimbiza mwanaume huyo aliyemshambulia kaka yake wakati alipokuwa akitoka nje ya ukumbi na kumpiga na kiatu.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote