Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, December 1, 2009

Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Mwanamke mmoja wa nchini Uingereza anayejulikana kwa jina la Emily Wallis alipigwa na mshangao wa mwaka alipogundua kuwa baba yake mzazi aliyekuwa akimtafuta kwa miaka mingi ni shoga na anavaa nguo za kike. Wakati Emily Wallis mwenye umri wa miaka 22 alipoamua kumtafuta baba yake ambaye hakuwahi kumuona tangia alipozaliwa, hakutarajia hata kidogo kumuona baba yake akivaa nguo za kike na viatu vya kuchuchumia kama yeye.Emily alipigwa na butwaa alipokutana na baba yake anayeitwa Clive Harrison kwa mara ya kwanza na kugundua baba yake huyo amekuwa shoga na anavaa nguo za kike na kujipodoa kama mwanamke.Baba yake ambaye amejipachika jina la kike la Chloe ana jumla ya pea 82 za viatu vya kike na ana nguo kibao za kike."Baba alikuwa amevaa gauni la rangi ya kijivu na alikuwa amejipaka vipodozi na kuvaa wigi, nilishindwa kupata kitu cha kusema zaidi ya kumsifia kwa kusema 'Unaonekana mrembo kuliko mimi'", alisema Emily."Kwa miaka mingi nilikuwa na ndoto ya kuwaunganisha tena baba na mama, lakini nilipomuona baba kwa jinsi alivyo sasa, nilijua ndoto yangu haiwezi kuwa ya kweli".Emily alianza kazi ya kumtafuta baba yake baada ya mama yake, Ann, kutoboa siri kuwa mwanaume aliyemlea sio baba yake halisi na kumwambia kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Clive wakati alipopata mimba yake.Katika kikao chao kwanza baada ya kukutana, Clive alimuambia binti yake kuwa alioa mara tatu lakini ndoa zake zote zilivunjika kutokana na matatizo yake ya kufanya ushoga kwa siri.Baada ya ndoa yake ya tatu kuvunjika aliamua kuweka wazi ushoga wake na kuanza kuvaa nguo za kike na baadae kujipa jina la Chloe wakati akisubiri kufanyiwa upasuaji wa kuziondoa nyeti zake za kiume na kupandikizwa nyeti za kike.Emily amefurahia kuungana na baba yake na ameridhia hali ya baba yake kiasi cha kwamba amemtaka awe mpambe wake wakati wa harusi yake.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote