
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Lady Jaydee Komando ameibuka na kuonyesha kusikitishwa kwake kwa kile ambacho hakutegemea mara baada ya video yake ambayo yeye mwenyewe kudai bado hajai release kuonyeshwa katika baadhi ya mitandao. Akiongea na moja ya chombo cha habari Jide alisema kuwa video hiyo bado hajawahi kuitambulisha wala kuitoa sehemu lakini anashangaa kuikuta kwenye baadhi ya mitandao ukiwemo Youtube. Wala sija release hiyo video lakini nashangaa ni nani ameamua kufanya hivyo, lakini yote kheri tu tunaendelea kukomaa mpaka tuone mwisho” alisema Jide kwa machungu.
No comments:
Post a Comment