Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, December 17, 2009

Mungu mlaze pema peponi Dk Lawrence Gama

KATIBU Mkuu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Lawrence Gama amefariki dunia jana asubuhi katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu. Habari ambazo Mwananchi ilizipata jana zilisema kuwa Dk Gama alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani. Hata hivyo, haikuweza kufahamika mara moja ni aina gani ya saratani iliyokuwa ikimsumbua kwa muda mrefu mwanasiasa huyo mwanzilishi wa CCM. Taarifa zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam zilisema kuwa Dk Gama alikuwa akipata matibabu kwa kwenda na kurudi nyumbani katika hospitali moja, iliyoko maeneo ya Victoria jijini Dar es Salaam. Lakini, hali yake ilibadilika ghafla na kulazwa katika zahanati hiyo kabla ya kukimbizwa Aga Khan kwa matibabu zaidi ambako alifariki dunia. Chanzo cha habari kilisema kuwa hadi jana asubuhi kabla ya umauti, marehemu alikuwa akipumua kwa kutumia mashine maalumu ya hewa ya oksijeni.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote