Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Wednesday, December 2, 2009

Afariki Baada ya kufanya Operesheni ya kupunguza makalio!!!!!

Miss Argentina wa mwaka 1994, Solange Magnano mwenye umri wa miaka 38 amefariki dunia baada ya kufanyiwa operesheni ya urembo ya kupunguza makalio.Solange ambaye ni mama wa watoto wawili mapacha, alifanyiwa operesheni hiyo siku ya alhamisi katika hospitali moja katika mji mkuu wa Argentina, Buenos Aires.Solange alitaka kufanya operesheni hiyo ili kupunguza ukubwa wa makalio yake na kuyatengeneza yawe katika shepu ya kuvutia.Aliwahishwa hospitali siku ya ijumaa akisumbuliwa na matatizo ya kuziba kwa mishipa ya damu na alifariki siku ya jumapili."Mwanamke huyu ambaye alikuwa mrembo mwenye kila kitu, amefariki kwasababu alitaka kuwa na makalio madogo", alisema Roberto Piazza, mbunifu wa mavazi na rafiki wa karibu wa Solange.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote