
Nyota namba moja duniani wa mchezo wa gofu, Tiger Woods amekiri kuisaliti ndoa yake na ameamua kustaafu kwa muda kucheza gofu baada ya wanawake 11 wakiwemo wacheza filamu za ngono kujitangaza kufanya naye mapenzi. Tiger Woods ameamua kustaafu kwa muda usiojulikana kucheza mchezo wa gofu baada ya idadi ya wanawake aliofanya nao mapenzi nje ya ndoa kuzidi kuongezeka.Jumla ya wanawake 11 wameishajitokeza na kujitangaza hadharani kuwa walifanya mapenzi mara kadhaa na nyota huyo maarufu duniani kwa mchezo wa gofu.Katika ujumbe aliouandika katika tovuti yake, Tiger Woods amekiri kuisaliti ndoa yake na amemuomba radhi mkewe Elin Nordegren kwa fedheha aliyomsababishia.Woods alisema kuwa anaamua kustaafu gofu kwa muda usiojulikana ili aweze kujishughulisha na familia yake akijifunza kuwa mume na baba mzuri.Hatua hiyo ya Woods imekuja kufuatia taarifa kuwa Woods alikuwa akitumia maelfu ya dola kuwahonga makahaba ghali wakati alipokuwa akishiriki kwenye matamasha ya gofu sehemu mbali mbali duniani.Taarifa zilisema kwamba ni mara chache sana Woods alichukua kahaba mmoja. Alikuwa akipenda kuona wanawake wakisagana hivyo karibia mara zote alikuwa akiwachukua makahaba wawili wawili.Woods pia amekuwa katika zengwe na Wamarekani weusi kufuatia madai kuwa alikuwa akipenda kujifanya mzungu na hakupenda wanawake weusi na ndio maana katika wanawake wote 11 waliojitokeza hakuna hata mwanamke mmoja mweusi.Woods amebaki peke yake hakuna nyota yoyote mweusi aliyemtetea huku baadhi ya madj katika redio za Marekani wamekuwa wakitoa maneno na rap za kebehi dhidi yake.Tiger, ambaye ana watoto wawili aliozaa na mkewe Elin, maisha yake ya ngono za siri akimsaliti mkewe yaligundulika kufuatia ajali isiyotegemewa nje ya nyumba yake.Katika ajali hiyo, Tiger Woods akiendesha gari lake kutoka nyumbani kwake kwenye majira ya saa nane usiku aligonga mti na kuzimia kwenye eneo la ajali hiyo.Taarifa zilizotolewa baadae zilisema kwamba Tiger Woods aliligongesha gari lake alipokuwa akimkimbia mkewe kufuatia mzozo wa mahusiano yake na mmoja wa wapenzi wake wa siri.Wadhamini wa Tiger Woods kama vile Pepsi, Gillette na Proctor and Gamble wapo kwenye majadialino ya kuendelea kumdhamini Woods au kumtosa.
No comments:
Post a Comment