Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, December 3, 2009

Watoto wa Michael waonyeshana umoja wa hali ya juu baina yao

Prince Michael II (Branket) akiwa na Kaka yake (mtoto wa Michael wa siri) Omer Bhatii


Mtoto mdogo wa Michael - Prince Michael II(Branket )

Prince akiwa na dada yake Paris

Mtoto Mkubwa wa Michael - Prince akitoka mazoezini
Inasemekana kuwa watoto wa Michael wamekuwa na mapenzi ya hali ya juu kati yao na kuonekana kuwa pamoja wakati wote mara baada ya baba yao kufariki, Kwa sasa watoto wa Michael wanaishi na bibi yao Katherini huko Encino Califonia toka Juni mara ya baba yao kufariki. Shangazi yao Latoya amesema kwa sasa watoto wamekuwa na wakati mgumu kutokana na kumpoteza baba yao. Latoya akizungumzia kuhusu wa watoto wa Michael alisema Mtoto mkubwa wa Michael, Prince Michael amekuwa na wakati mgumu sana ukilinganisha na wenzake na hataki kuzungumza na kukubali kuhusu kifo cha baba yake, Latoya aliongeza kuwa Prince Michael na mdogo wake Prince Michael II wanasumbuliwa na ugonjwa wa Vitiligo (ugonjwa wa ngozi) ambao baba yao alikuwa nao. Akimzungumzia Blanket (mtoto mdogo wa Michael) Latoya amesema mtoto huyo alimzoea sana baba yake kwa sasa amekuwa na muda mgumu pia kiasi kwamba kuna muda unaona ana huzuni na kulia mara kwa mara na hii imesababishwa na ule ukaribu na mapenzi kwa baba yake “inauma sana kwa sababu hatuwezi kumrudisha baba yake” alisema Latoya, pia alimuelezea Blacket kuwa ni mtoto mwenye aibu sana. Kwa upande wa Paris anasema Paris amekuwa mvumilivu muda wote na anajitahidi kukubaliana na ukweli wa kifo cha baba yake . Paris kila wakati humuwaza na hupenda kuongea kuhusu baba yake .


No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote