Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Wednesday, December 2, 2009

Hatimaje Mfungwa atunukiwa shahada ya Sheria akiwa gerezani


Mfungwa Semayoga Ernest (30), ametunukiwa Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT). Alitunukiwa shahada hiyo na Mkuu wa OUT, John Malecela, katika hafla ya kutunikiwa shahada hiyo ilifanyika kwenye viwanja vya Kikosi Maalum Ukonga jana. Ernest aliomba serikali kuangalia uwezekano wa kuanzisha sekondari gerezani ili kusaidia wafungwa wasio na sifa za kujiunga na chuo. Mfungwa huyo anatumikia kifungo cha miaka 10. Ernest aliahidi kutumia shahada hiyo kutoa mafunzo kwa wafungwa wenzake wanaohitaji msaada wa kisheria. Alisema licha ya serikali kukubali ombi la OUT kuanzishwa kwa chuo hicho gerezani humo, iangalie wafungwa ambao hawajapata nafasi za masomo ya sekondari. "Baadhi ya wafungwa wamekuwa wakifungwa kwa kutojua sheria vizuri, hivyo kwa kutumia shahada niliyoipata nitatoa msaada wa kisheria kwa wenzangu ili waweze kujitetea, naamini watafahamu haki zao na kufanikiwa," alisema. Aliongeza kuwa elimu aliyoipata haina maana kuwa ndio mwisho bali lengo lake, ni kusoma shahada ya uzamili kwenye fani hiyo ili aweze kuwa mwanasheria wa kujitegemea. Sherehe hizo zilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, Kamishna wa Magereza, Augustino Nanyaro, Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Tolly Mbwete na mfungwa mwenzake Haruna Pembe ambaye kwa sasa anasoma Shahada ya Uzamili katika sheria chuoni hapo. Waziri Masha alisema serikali imeanza kutafuta fedha kwa kwa taasisi mbalimbali iweze kutoa elimu zaidi kwa wafungwa gerezani kwa kushirikiana na chuo hicho. Masha alisema shahada ya Ernest ni changamoto kwa jamii kuwa gerezani sio mahala pabaya, bali ni sehemu ambayo mtu anabadilishwa kulingana na kosa lililomfikisha.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote