Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, December 14, 2009

Gari ya Mashindano laua watoto 5


WATU watano wamekufa, kati yao wanne papo hapo, baada ya gari la mashindano ya mbio za magari kuacha barabara na kuparamia umati wa watu waliojipanga kando kando ya njia eneo la Mikese Njianne, wilayani Morogoro. Ajali hiyo imesababisha pia majeruhi 12 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Gari hilo lenye namba za usajili kutoka Kenya KAK 9208 aina ya Subaru likiwa miongoni mwa magari 16 yaliyoshiriki, liliandikishwa namba sita ya katika mashindano ya mbio za umbali wa kilometa 380 yajulikayo kwa jina la Morogoro Pathfinder Rally 2009 na iliendeshwa na dereva Dharam Pandya( 29). Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ferdinand Mtui, alithibitisha kuwa ajali hiyo ilitokea jana saa 4:30 asubuhi eneo la Mikese Njianne kwenye barabara ya vumbi. Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda huyo, watu waliokufa kwenye ajali hiyo ni watoto wenye umri kati ya miaka sita na kuendelea waliokuwa miongoni mwa watazamaji wa mashindano hayo. Alisema ajali hiyo katika barabara ya vumbi mara baada ya kufika Mikese Mizani, ambapo magari hayo yalitumia barabara ya kawaida na gari hilo lilipofika eneo lenye kona liliacha njia na kuwaparamia watu na kupinduka na hivyo kusababisha vifo hivyo na majeruhi hao. Kati ya maiti hizo nne mmoja ndiye iliyotambuliwa kwa jina la Jacob Mashaka ( 6) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Awali katika Kijiji cha Mikese. Naye Ofisa wa zamu katika Hosptitali ya Mkoa wa Morogoro, Judith Kagimbwa, alithibitisha kupokea majeruhi 12 na miili minne. Alisema majeruhi mwingine alifariki akiwa wodini saa 7:30 mchana. Naye ni Said Mohamed ( 40) . Majeruhi 11 wanaoendelea kupatiwa matibabu ni Pamela Ashumba ( 50), Mgema Deus (16), Mwanaidi Rajab (21), Iddi Hamis ( 40), Hadija Mwarabu (28), Mwamini Said (28), Juma Abdallah (33), Alex Mussa (14) Daniel Masanja (12) na Shukuru Roma (28) ambao baadhi yao ni wakazi wa Mikese na wengine nje ya Mikese.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote