Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, December 8, 2009

Apigwa hadi kupoteza Fahamu kisa kumpiku MUMEWE kwenye Uchaguzi

MWANAMKE Salma Musa mkazi wa Kiloleni Mkoani Tabora, amelazwa katika hospitali ya Mkoa huo baada ya kupigwa na mumewe hadi kupoteza fahamu kwa kile kinachosemekena kushinda uchaguzi wa Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa kwa tiketi ya CCM. Mwanamke huyo alipigwa baada ya kumpiku mumewe huyo katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni nchini kote ambapo yeye aligombania kiti hicho kwa tiketi ya CCM na mumewe huyo kugombania kiti hicho kwa tiketi ya CUF.Akielezea mkasa huo kwa waandishi wa habari kwa shida, huku akiwa kitandani katika hospitali hiyo, baada ya kupata fahamu kidogo Salma alisema kuwa sababu iliyomfanya apigwe na mume wake huyo kukerwa na kitendo cha yeye kushinda uchaguzi huo kwa tiketi ya CCM.Alieleza kuwa mume wake huyo alikuwa akimkorofisha kwa muda mrefu na kukerwa na kitendo cha yeye kumpiku katika uchaguzi huo na kusema kuwa yeye alitoa rushwa kwa wasimamizi wa uchaguzi na maneno mengi kuashiria hakushinda kwa halali kwenye uchaguzi huo lazima atakuwa ametoa rushwa ya ngono kwa wasimamizi.Alisema mara kwa mara alikuwa akimpiga lakini alimsihi kuwa aachane na tabia hiyo lakini aliendela na vitendo vya kumpiga mara kwa mara na mara ya mwisho alimwamia kuwa akimpiga anakimbilia polisi kutoa taarifa.Alisema baada ya kumwambia hiyo ndipo alimpiga hadi kupelekea kupoteza fahamu na majirani kukimblia polisi kutoa taarifa kufuatia tukio hilo.Mkuuu wa Wilaya ya Tabora Mussa Chang’a amesema kuwa mume wa dada huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kufuatia ukatili huo alioufanya kwa mke wake huyo.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote