Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Wednesday, December 9, 2009

Mtoto wa Chenge mbaroni kwa kusababisha Ajali

Madina Chenge (25), mkazi wa Oysterbay, jijini Dar es Salaam anayedaiwa kuwa mtoto wa Mbunge wa Bariadi Magharibi, mkoani Shinyanga, Andrew Chenge (CCM), amefikishwa mahakamani kujibu shitaka la kuendesha gari bila kuzingatia sheria za usalama barabarani. Madina alifikishwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam na shitaka lake liko mbele ya Hakimu Samuel Maweda wa mahakama hiyo. Awali hati ya shitaka iliyosomwa mahakamani hapo ikidai kuwa mshitakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa Novemba 17, mwaka huu saa 11:30 jioni katika makutano ya barabara ya Umoja wa Mataifa na ya Mt. Imaculata, jijini Dar es Salaam.Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa siku ya tukio hilo, mshitakiwa aliendesha vibaya gari lililokuwa na namba za usajili T 193 AYL aina ya Toyota Harrier kwenye barabara hizo na kushindwa kusimama alipofika kwenye barabara ndogo ya Mt. Imaculata.Ilidaiwa kuwa shitakiwa huyo alitakiwa kusimama ili kutoa nafasi kwanza kwa shughuli za kitrafiki katika barabara kuu ya Umoja wa Mataifa kumalizika, lakini matokeo yake mshitakiwa alidaiwa kuendesha gari vibaya bila kufuata taratibu hizo za kitrafiki na kugongana na gari lenye namba za usajili T 958 ATS aina ya Toyota Land Cruiser na kusababisha uharibifu katika magari yote mawili. Hata hivyo, Madina alipewa dhamana ambayo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili waliotakiwa kusaini dhamana ya Sh. 500,000 kila mmoja kwa kiwango hicho. Kesi hiyo iliyotajwa kwa mara ya kwanza Novemba 24, mwaka huu, lakini waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuiripoti. Kesi hiyo iliahirishwa na itatajwa tena mahakamani hapo kesho. Madina anakabiliwa na kesi hiyo huku baba yake, Andrew Chenge (61), akikabiliwa na kesi ya kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha ajali iliyoua wasichana wawili jijini Dar es Salaam, baada ya gari lake kuigonga bajaj Machi, mwaka huu.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote