Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Tuesday, December 1, 2009

Kesi ya Familia ya NGUZA watu wasema Mnyonge Mnyongeni ila Haki yake Mpeni

Katika rufaa ya kesi hiyo iliyovuta umati wa wasikilizaji katika mahakama hiyo, ilianza kuunguruma majira ya saa tatu asubuhi ikiwa na jopo la majaji watatu, Mbarouk Salim, Salum Massati pamoja na Nathalia Kimaro, aliyekuwa akiliongoza jopo hilo. Kabla ya rufaa ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa, ndugu na jamaa wa familia hiyo walianza kuangua vilio mahakamani hapo baada ya kumuona Babu Seya na wanaye, Papii Kocha, Nguza Mbangu na Francis Nguza wakiamrishwa kushuka kwenye karandinga lenye nambari za usajili STG 6355 na maafande wa magereza. Mwanamke mmoja aliyekuwa miongoni mwa waliokuwa wakiangua kilio katika viunga vya mahakama hiyo alisema kuwa, kilichomtoa machozi ni hali za wapendwa wao hao ambao alikuwa hajawaona tangu walipotiwa hatiani, Juni 25, mwaka 2004. Mwanadada huyo alidai kuwa, Babu Seya na wanaye wamezeeka kwa asilimia ishirini na tano ukilinganisha na hali waliyokuwa mwaka 2004 kabla ya kuswekwa gerezani. Baada ya kupandishwa kizimbani, wakili anayewatetea wakata rufaa hao, Mabere Marando, aliiomba Mahakama hiyo isogeze mbele rufaa kwani awali ilikuwa chini ya Wakili Albert Nyange kabla ya kukabidhiwa kwake Novemba 27, mwaka huu. Marando alidai kuwa, muda waliopewa ni mfupi mno hivyo kuiomba mahakama kutoa muda zaidi ili kuichambua kesi hiyo kwa ajili ya kuwatetea wateja wake. Marando ambaye kabla ya kuanza kusikilizwa rufaa hiyo, aliongeza sababu zaidi za rufaa hiyo ambapo zilifikia jumla ya sababu 19 pamoja na sababu zilizowasilishwa awali na Wakili Nyange. Wakili Mkuu wa Serikali katika Rufaa hiyo, Justus Mulokozi alikubaliana na Marando katika hoja hiyo na kusema kuwa hata yeye ameshindwa kuzipitia sababu zilizoongezwa na Marando kwani zimemfika muda mfupi kabla ya kuanza rufaa hiyo. Baada ya Wakili Mkuu wa Serikali kukubaliana na hoja ya Marando, Jaji aliyekuwa akiliongoza jopo hilo, Nathalia Kimaro, aliiahirisha kesi hiyo hadi Desemba 3, mwaka huu, ambapo wakata rufaa hao watafikishwa tena mahakamani hapo ambapo Babu Seya na wanaye walirejeshwa katika Gereza la Ukonga. Hii ni rufaa ya pili kwa kesi hiyo ya Babu Seya na wanaye, baada ya ile ya kwanza iliyowasilishwa mwaka 2005 kukataliwa mbele ya Jaji Thomas Mihayo wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambaye aliikataa na kukubaliana na hukumu iliyotolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Addy Lyamuya, Juni 25, 2004

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote