Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Wednesday, December 9, 2009

Uongozi Dar waipiga Stop MAJEMBE kushugulikia Daladala

Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, umesimamisha kwa muda shughuli za kampuni ya Majembe Auction Mart za kukamata magari ya daladala ambayo yanakiuka taratibu na sheria za barabarani. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kubainika kuwepo kwa mapungufu mbalimbali ikiwemo ukinzani wa kisheria katika utekelezaji wa agizo hilo, jambo ambalo badala ya zoezi kuwa na manufaa, limegeuka kuwa kero. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, alisema zoezi hilo limesitishwa ili kutoa nafasi kwa wenye magari kujipanga upya kutimiza masharti ya usalama barabarani badala ya kulazimishana. Kampuni ya Majembe ilianza kukamata daladala zinazokiuka sheria wiki iliyopita baada ya kuingia katika mkataba wa mwaka mmoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra). Hadi kufikia jana, zaidi ya daladala 400 zilishakamatwa na kutozwa faini kwa makosa mbalimbali, ambapo faini hizo zilikuwa zikilalamikiwa na wamiliki wa daladala kuwa ni kubwa. Faini hizo zilikuwa ni kati ya Sh. 200,000 na 250,000 hatua ambayo iliwafanya madereva kugoma kutoa huduma hiyo juzi katika maeneo ya Tabata, jijini Dar es Salaam.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote