Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, December 14, 2009

Kikongwe cha miaka 98 chaau kikongwe cha miaka 100

Bibi mwenye umri wa miaka 98 wa nchini Marekani amefunguliwa mashtaka ya mauji kwa kumuua bibi mwenye umri wa miaka 100 aliyekuwa akiishi naye chumba kimoja kwenye nyumba ya kutunza vikongwe. Bibi Laura Lundquist mwenye umri wa miaka 98 anakabiliwa na kesi ya mauaji ya bibi mwenzake mwenye umri wa miaka 100. Bibi Laura anatuhumiwa kumziba pumzi mpaka kumuua bibi Elizabeth Barrow aliyekuwa akiishi naye chumba kimoja kwenye nyumba ya kutunza vikongwe iliyopo Massachusetts nchini Marekani. Jaji wa kesi hiyo ameamuru bibi Laura apelekwe hospitali kwanza kupimwa akili zake kabla kesi hiyo haijaendelea. Katika tukio hilo lililotokea septemba 24, Bibi Elizabeth alikutwa amefariki chumbani kwake huku mfuko wa plastiki ukiwa juu ya kichwa chake. Mtoto wa kiume wa bibi Elizabeth, Scott Barrow alisema kuwa bibi Laura alikuwa akimtishia maisha mama yake mara kadhaa alipokuwa akimtembelea kwenye nyumba hiyo.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote