.jpg)
Mchungaji huyo wa kanisa la kijiji cha Makurunge, inadaiwa alitekwa juzi. Kaka wa mchungaji huyo, Bw. Emmanuel Ntungu ameyaambia baadhi ya magazeti kuwa tangu jana usiku yuko na askari polisi wakijaribu kumtafuta ndugu yake ambaye inadaiwa amefichwa na watekaji kwenye jumba moja lililo karibu na bahari. “Jana niliitwa polisi wakanihoji na jioni waliandika maelezo…ndipo kazi ya kuanza kumsaka ikaanza lakini hadi sasa hatujaambulia kitu,’’ amesema.Amesema ndugu zao wengine wameanza kuzunguka kwenye hospitali mbalimbali na vituo vya usalama kujaribu kumtafuta Mchungaji Michael. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Mark Kalunguyeye, amesema bado wanafuatilia tukio hilo.
No comments:
Post a Comment