Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Monday, December 14, 2009

Majaji Miss Tanzania angalieni vigezo upya la sivyo itakuwa ni watu wa kusindikiza kila siku

Miss Dunia mwaka 2009 Kaiane Aldorino

MASHINDANO ya kumtafuta mrembo wa dunia yamefanyika jana huko Johannesburg, Afrika Kusini huku mrembo wa Tanzania akitoka mikono mitupu katika mashindano hayo. Katika mashindano hayo mwaka huu Tanzania iliwakilishwa na mrembo Miriam Gerald, ambaye amekuwa ni mrembo wa 16 wa Tanzania kuwania taji hilo tangu mwaka 1994. Mrembo Nany Sumari ndiye pekee aliyeweka rekodi nchini kwa kuibuka na taji la Afrika au Miss World Africa mwaka 2005 kwa kuwa miongoni mwa warembo watano bora duniani. Mashindano hayo ya 59 ya kumtafuta mrembo wa dunia mwaka huu yalishirikisha warembo 112, ambapo mrembo kutoka Gibraltar anayeitwa Kaiane Aldorino ndiye aliyeibuka mshindi. Tunapenda kumpongeza Miriam kwa kujitahidi kuliwakilisha Taifa ingawa hakufanikiwa kufanya vizuri katika mashindano hayo. Tunatarajia waandaaji wa Miss Tanzania watakuwa wamejiunza mengi katika mashindano hayo ya dunia na watajitahidi kuboresha mashindano yetu.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote