Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Friday, December 4, 2009

Wabomoa Kaburi la Bilionea na kuiba maiti

Wanaume wawili wamekamatwa nchini Hungary wakituhumiwa kulilipua kaburi la aliyekuwa bilionea wa Ujerumani Friedrich Karl Flick na kisha kuliiba jeneza lake likiwa na mwili wake.Wanaume hao wamekamatwa kufuatia msako uliokuwa ukiendelea katika nchi za ulaya wakati "Wezi wa Maiti" kama walivyokuwa wakijiita walipodai walipwe fidia ya dola milioni 9.8 toka kwa familia ya bilionea huyo ndipo waurudishe mwili wake."Wahalifu hawa walitaka walipwe euro milioni 6 lakini walilipwa euro laki mbili na familia ya bilionea Flick", alisema afisa wa makosa ya jinai wa Austria, Ernst Geiger.Polisi wa Budapest, Hungary walitangaza siku ya jumatano kuwa wamewakamata wanaume wawili na wanawatafuta wanaume wengine wawili kuhusiana na wizi wa jeneza la Flick ambalo lilipatikana siku ya jumapili nchini humo.Jeneza la Flick likiwa na maiti yake liliibwa toka kwenye kaburi lake novemba mwaka jana katika mji wa Velden, Kusini mwa Austria baada ya wezi kulilipua kaburi lake kwa baruti.Mwezi mmoja baadae mjane wa bilionea Flick alitangaza zawadi ya dola 160,000 kwa mtu atakayeirudisha maiti yake.Jeneza lake inasemekana lilisafirishwa kwa lori toka Australia baada ya kufukuliwa na kuingizwa kisiri nchini Hungary.Mwishoni mwa mwezi uliopita, polisi wa Hungary walifanikiwa kuvipata vipande vya jeneza lake katika sehemu mbili tofauti za mji wa Budapest. Flick alifariki mwaka 2006 akiwa na umri wa miaka 79. Wakati anafariki kwa mujibu wa jarida la Forbes, alikuwa akishikilia nafasi ya 94 kwa utajiri duniani.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote