

Majonzi na huzuni vimetawala wakati wa kumuaga aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya The Guardian Limited, marehemu Vumi Urasa, kwenye misa maalumu iliyofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Magomeni jijini Dar es Salaam. Urasa alifariki dunia Jumanne wiki hii kwenye Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam . Baada ya mwili wake kuagwa ulisafirishwa kwenda Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yatakayofanyika leo. Marehemu Urasa ameacha mke, watato watatu na mjukuu mmoja.
No comments:
Post a Comment