Uwepo wa Site hii Unategemea sana Ushirikiano wangu na wako, na ni njia mojawapo ya kuonyesha mshikamano na Jamii inayotuzunguka , PLS Usisite kunitumia Habari au kitu chochote chenye Uhakika ambacho hisia zako zitakupeleka kuwa kitaleta Mabadiliko na mafunzo katika jamii, Kumbuka kuwa msaada si Fedha wala Lulu bali chochote kinachoweza kuleta mabadiliko katika Maisha ya mtu mwingine. Kwa lolote usisite kuwasiliana nami kupitia chingasite@gmail.com au tumainijhn@yahoo.co.uk au simu No. 0712221744 na 0787221744. Karibuni Wote
Powered By Blogger

Thursday, December 17, 2009

Ugumu wa maisha wamfanya auwe watu ili ahukumiwe kunyongwa

Mwanaume mmoja wa nchini China ambaye alikuwa na nia ya kujiua baada ya kushindwa kupata kazi kwa muda mrefu, amewaua watu wawili ili ahukumiwe kunyongwa. Mwanaume huyo alikuwa na nia ya kujiua lakini alikuwa hana ujasiri wa kuitoa roho yake mwenyewe. Aliamua kuwaua watu wawili ili ahukumiwe adhabu ya kunyongwa.Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye alitajwa kwa jina moja tu la Bin, alichukua uamuzi huo kutokana na hali ngumu ya maisha aliyokuwa nayo baada ya kushindwa kupata kazi kwa muda mrefu.Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya mji wa Jiangmen katika jimbo la Guangdong, Bin aliwaua watu wawili kwa kuwanyonga ili ahukumiwe adhabu ya kifo."Bin alisema Kwa muda mrefu sina kazi, sina uwezo wa kujiua mwenyewe, nimefanya mauaji ili nihukumiwe kunyongwa", .Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na polisi, Bin hana uhusiano wowote na wala alikuwa hawajui watu aliowaua.

No comments:

VJN Super Motors

Wauzaji Mahiri wa Spare za Pikipiki na Magari yote toka Europe na Japan, Tupo Mtaa wa Msikitini Musoma Mjini, Pia tunaweza kutoa hudumu kwa watu wa Dar es salaam, Wasiliana nasi kwa Sanduku la Barua 557 Musoma, Simu No. 0282620610 , Barua pepe : vincent_nye@yahoo.co.uk. Karibuni wote